NICKI MINAJI ATAKIWA KULIPA BILIONI 13 – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

 

Nicki Minaj anaingia kwenye mzozo wa kisheria na shabiki ambaye alimtaja hadharani kuwa hana akili timamu na mviziaji.

 

 

Mwimbaji huyo wa kike mwenye umri wa miaka 41, ambaye jina lake halisi ni Onika Tanya Maraj, si mgeni katika mabishano, mara nyingi alijikuta katikati ya mizozo ya watu mashuhuri, ikiwa ni pamoja na ugomvi wake maarufu na Megan the Stallion.

 

 

 

Sasa nyota huyo anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama kuu ya Los Angeles, kwa kumkejeli Tameer Peak kuwa ana matatizo ya akili na ni mviziaji.

 

Peak anadai kuwa amekuwa mmoja wa mashabiki waaminifu zaidi wa Nicki kwa miaka 15 iliyopita na anadai alishiriki katika kutangaza Pink Friday 2, albamu yake iliyotoka hivi karibuni.

 

 

Kwa mujibu wa TMZ, Peak anadai licha ya kuwa shabiki mkubwa bado Nicki amekuwa akimdhalilisha na kumkejeli tangu mwaka 2017 , hivyo anadai fidia ya $5 Milion zaidi ya Tsh Bilion 13 kwa kumchafua na kuharibu jina lake.

Related Posts