Rais Abdelmadjid Tebboune ashinda muhula wa pili Algeria – DW – 09.09.2024

Katika matokeo ambayo yaliwashangaza waangalizi wachache kimataifa na hata ndani ya Algeria kwenyewe, tume huru ya uchaguzi nchini humo ilitangaza Jumapili kwamba Tebboune ameshinda asilimia 94 ya kura, akiwazidi wapinzani wake, mgombea wa chama cha Kiislamu, Abdelali Hassani Cherif, aliyepata asilimia 3 pekee na msoshalisti Youcef Aouchiche, ambaye aliambulia asilimia 2.1.

Maafisa wa uchaguzi wameripoti kuwa chini ya milioni sita kati ya wapiga kura milioni 24 nchini humo walijitokeza kupiga kura siku ya Jumamosi, na kuendeleza viwango vya chini vya wapiga kura ambavyo viliathiri muhula wa kwanza wa Tebboune na kuibua maswali kuhusu uungwaji mkono wake wa umma.

Soma pia: Raia wa Algeria wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais

Jumla ya mgao wa kura za Tebboune ulikuwa zaidi ya asilimia 87 ambazo Vladimir Putin alishinda katika uchaguzi wa Machi wa Urusi na asilimia 92 ambayo Ilham Aliyev alipata katika uchaguzi wa Februari nchini Azerbaijan. Waangalizi huru hawakuruhusiwa nchini Urusi wala Algeria.

Algeria | Rais Abdelmadjid Tebboune
Rais Tebboune aliingia madarakani kwa mara ya kwanza Desemba 2019, baada ya mtangulizi wake Abdel-Aziz Bouteflika kuondolewa na jeshi kufuatia maandamano ya kuda demokrasia.Picha: Xinhua News Agency/picture alliance

Tofauti ya ushindi wa Tebboune imepita kwa mbali ushindi wake wa 2019, aliposhinda asilimia 58 ya kura na mpinzani wake wa karibu akipata asilimia 17. Maafisa walikuwa bado hawajatangaza idadi rasmi ya waliojitokeza kufikia Jumapili alasiri, ingawa jumla ya awali haikulingana na takwimu za muda zilizotangazwa Jumamosi usiku, ambapo tume ya uchaguzi ilisema waliojitokeza kupiga kura walikuwa asilimia 48 ndani ya Algeria na asilimia 19.6 kwa maeneo ya nje ya nchi.

Algeria ndiyo nchi kubwa zaidi barani Afrika kwa eneo la kijiografia na, kwa idadi ya watu karibu milioni 45, ndiyo taifa la pili kwa idadi kubwa ya watu baada ya Afrika Kusini kufanya uchaguzi wa rais mwaka huu wa 2024 – mwaka ambao zaidi ya chaguzi 50 zinafanyika kote ulimwenguni, zikijumuisha zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani.

Mazingira ya ukandamizaji kuelekea uchaguzi

Katika wakati wote wa kampeni, wanaharakati na mashirika ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Amnesty International, walikosoa mazingira ya ukandamizaji ya msimu wa kampeni na unyanyasaji na utesaji wanachaa wa vyama vya upinzani, mashirika ya vyombo vya habari na mashirika ya kiraia. Baadhi walipuuza uchaguzi huu wakiutaja kama zoezi la kukamilisha tu ratiba, ambalo inaweza tu kuendeleza na kuimarisha hali iliyopo.

Algeria I Uchaguzi wa rais 2024
Mgombea wa upinzani Abdelali Hassani Cherif kutoka chama cha Movement of Society for Peace (MSP), akipiga kura yake siku ya uchaguzi. Cherif ameambulia asilimia tatu tu ya kura.Picha: Fateh Guidoum/AP/picture alliance

Lakini Tebboune na wapinzani wake wawili kila mmoja alihimiza ushiriki wa kisiasa na hasa kufanya mabadiliko kwa vijana wa Algeria, ambao ni sehemu kubwa ya wakazi na wanaoteseka kwa wingi kutokana na umaskini na ukosefu wa ajira.

Soma pia: Algeria yamuapisha rais mpya anayepingwa na waandamanaji

Takriban nusu ya wapiga kura katika taifa hilo lenye utajiri wa gesi Kaskazini mwa Afrika walipiga kura, Tume Huru ya Uchaguzi ilisema saa chache baada ya uchaguzi kufungwa. Idadi ya awali iliyoripotiwa inazidi ushiriki wa  waliojitokeza kupiga kura kutoka miaka mitano iliyopita, wakati Abdelmadjid Tebboune aliposhinda uchaguzi wake wa kwanza, katika kinyang’anyiro kilichosusiwa kwa sehemu kubwa na waandamanaji wa kudai demokrasia, ambao maandamano yao ya kila wiki yalipelekea kupinduliwa kwa mtangulizi wake.

Ushiriki wa juu zaidi lilikuwa lengo lililotangazwa sana kwa Tebboune na wapinzani wake wawili. Kila mmoja wa wagombea hao watatu alihimiza ushiriki wa kisiasa huku wanaharakati wengine na vyama vya siasa wakitoa wito wa kususia tena, wakihofia uchaguzi huo ungeimarisha tu hali ya sasa.

Turakella: Ubaguzi nchini Algeria ulifungua mlango wa fursa

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Kabla ya maafisa kutangaza ushindi huo mkubwa wa Tebboune, wapinzani wake walinung’unika kuhusu ucheleweshaji na kudai kuwa kulikuwa na kasoro za jinsi rekodi zilivyoripotiwa kwa umma na ofisi za kampeni za wagombea.

Katika taarifa ya Jumapili, Ahmed Sadok, meneja wa kampeni wa mgombea wa Kiislamu Abdelali Hassani Cherif aliangazia ratiba hiyo na kudai kuwa kumekuwa na kushindwa kuwasilisha rekodi za kupanga kura kwa wawakilishi wa wagombea.

Alisema Movement of Society for Peace, chama cha Cherif chenye msimamo wa wastani wa Kiislamu kilirekodi matukio ya upigaji kura wa vikundi vya uwakala na shinikizo lililowekwa kwa wafanyakazi wa uchaguzi ili kuongeza idadi fulani, ambayo hakikuiainisha.

Related Posts

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi ▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi ▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio ▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini Dar es Salaam Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo ikiwemo upunguzaji wa ada ya pango kwa mwaka ya leseni (Annual Rent) za uchimbaji mdogo wa chumvi nchini ili kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuchochea uzalishaji wa wingi wa chumvi nchini. Hayo yamesemwa jana tarehe 15 Julai, 2025 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Kikao cha wadau wa sekta ndogo ya chumvi chini ya Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA). "*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kutubeba sekta ya madini na wachimbaji kwa ujumla. Ni yeye aliyetuelekeza kusikilize kilio chenu na kutatua changamoto zinazowakabili ili mnufaike na shughuli mnazofanya" "Ametuelekeza Wizara ya Madini tuliridhie ombi lenu na kupunguza ada ya pango ya mwaka ya leseni ya uchimbaji mdogo kutoka Shilingi 45,000 mpaka Shilingi 20,000 kwa hekta, hili linakwenda kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ubora wa chumvi ya mzalishaji mdogo" alieleza Mhe. Mavunde. Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo udhibiti wa chumvi inayoingizwa kutoka nje ya nchi, zimepelekea bei ya chumvi ghafi kuongezeka na hivyo kuwanufaisha zaidi wazalishaji wadogo wa chumvi nchini. Uanzishwaji wa kodi ya zuio ya asilimia mbili (2%) kwenye mauzo ya chumvi ghafi kwa wazalishaji wenye leseni za PML imekuwa ni neema na manufaa kwao badala ya utaratibu wa awali wa kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato, ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wazalishaji wadogo. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde alieleza kuwa Kiwanda cha kuzalisha chumvi cha STAMICO kipo hatua za mwisho, na kuagiza Shirika hilo kuhakikisha kabla ya mwezi wa Agosti kuisha kiwe kimekamilika na kuanza uzalishaji wa chumvi ili kupanua wigo wa soko la chumvi ya wazalishaji wadogo. Awali, akitoa taarifa ya utendaji wa Taasisi yao, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia aliishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto zilizokuwa zinaikabili sekta ndogo ya chumvi nchini ambazo zimepelekea bei ya chumvi kupanda na kuwanufaisha zaidi wazalisha chumvi nchini.