KUPIKA KWA NISHATI SAFI YA PUMAGAS KUNASAIDIA ULINZI WA MAZINGIRA

Na Mwandishi Wetu

Katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, Kampuni ya Puma Energy Tanzania kupitia PumaGas imezindua kampeni ya Bei kama Mkaa faida kibao yenye lengo la kuwahimiza wananchi kupika kwa nshati ya gesi.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika leo Septemba 10, 2024 katika Viwanja vya Zakhem, Mbagala mkoani Dar es Salaam ambapo pia wananchi wameelimishwa kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia hususan ya PumaGas ambayo ni rafiki wa usafi na mazingira.

Akizungumza katika kampeni hiyo Meneja Masoko wa Puma Energy Tanzania, Lilian Kanora amesema kampeni hiyo inalenga kuelimisha jamii na kuhimiza matumizi ya nishati safi kwani PumaGas inaokoa muda wa mama katika kupika, pia inatoa uhakika kwa mama kutoathirika kiafya kwa kuvuta moshi mwingi akiwa jikoni anapika.

Ameongeza kuwa kupika kwa nishati safi ya PumaGas kunasaidia ulinzi wa mazingira kwani hakutakuwa na sababu ya baba au mama kwenda kukata kuni porini na kuharibu mazingira.

Akieleza zaidi amesema kampeni hiyo inalenga kumhakikisha mwananchi kutumia fedha kidogo katika kununua nishati safi ukilinganisha na fedha anayotumia kununua Mkaa.

“Nitawapa mfano kopo moja la mkaa ni Sh1000 hadi Sh.2000 na kwa familia inayopika milo mitatu kwa siku hii ni sawa na Sh.2000 hadi Sh.4000 kwa siku.

“Ukipiga hizi hesabu kwa mwezi ni zaidi ya Sh.60,000 wakati PugaGas kilo sita ni Sh.41000. Katika kampeni hii kutakuwa na punguzo la bei kqa mtungi wa kilo 15 awali mteja alikuwa akipata gesi na mtungi mpya kwa Sh.75000 ila kwa kipindi hiki kuna punguzo hadi Sh.66000.

“Mtungi wa kilo sita utapatikana kwa Sh.41000 tu na mtungi wa kilo 38 pamoja na gesi unapatikana kwa Sh.110,000,”amesema na kusisitiza Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeweka mkakati maalum wa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Amesisitiza kuwa Puma Energy Tanzania imekuwa na Serikali nyakati zote katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia na wameshiriki vikao vyote vinavyozungumzia nishati hiyo na kinachofanyika katika kampeni ya Bei kama Mkaa faida Kibao ni kuonesha kwa vitendo dhamira yao ya kufanikisha mikakati ya nahati safi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mauzo PumaGas katika Kampuni ya Puma Energy Tanzania Jeffrey Nasser ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wote kuunga mkono kampeni hiyo huku akishauri hasa wanaume kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa kuwezesha familia kutumia nishati safi ya kupikia ya PumaGas.

“Nitoe rai kwa wanaume ambao ndio baba wa familia,kuna msemo wa baba ni kichwa cha familia basi sasa wanaponunua mahitaji ya nyumbani yakiwemo ya chakula wahakikishe wananunua na nishati safi ya kupikia.

Akizungumza kuhusu mikakati ya kuhakikisha PumaGas inafika kwa wananchi wengi amesema baada ya kuanza na mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanaendelea kutanua wigo na siku za karibuni watafikisha huduma ya mitungi ya PumaGas Dodoma na maeneo mengine na kufafanua PumaGas inapatikana kwa mawakala wao pamoja na vituo vya mafuta vya Puma.

Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa Mbagal na Pwani ambao wameshiriki katika uzinduzi wa kampeni hiyo wamesema wanatambua juhudi za Rais Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia hivyo nao wanamuunga mkono na wameshaachana na matumizi ya kuni na mkaa.

Related Posts

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi ▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi ▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio ▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini Dar es Salaam Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo ikiwemo upunguzaji wa ada ya pango kwa mwaka ya leseni (Annual Rent) za uchimbaji mdogo wa chumvi nchini ili kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuchochea uzalishaji wa wingi wa chumvi nchini. Hayo yamesemwa jana tarehe 15 Julai, 2025 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Kikao cha wadau wa sekta ndogo ya chumvi chini ya Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA). "*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kutubeba sekta ya madini na wachimbaji kwa ujumla. Ni yeye aliyetuelekeza kusikilize kilio chenu na kutatua changamoto zinazowakabili ili mnufaike na shughuli mnazofanya" "Ametuelekeza Wizara ya Madini tuliridhie ombi lenu na kupunguza ada ya pango ya mwaka ya leseni ya uchimbaji mdogo kutoka Shilingi 45,000 mpaka Shilingi 20,000 kwa hekta, hili linakwenda kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ubora wa chumvi ya mzalishaji mdogo" alieleza Mhe. Mavunde. Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo udhibiti wa chumvi inayoingizwa kutoka nje ya nchi, zimepelekea bei ya chumvi ghafi kuongezeka na hivyo kuwanufaisha zaidi wazalishaji wadogo wa chumvi nchini. Uanzishwaji wa kodi ya zuio ya asilimia mbili (2%) kwenye mauzo ya chumvi ghafi kwa wazalishaji wenye leseni za PML imekuwa ni neema na manufaa kwao badala ya utaratibu wa awali wa kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato, ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wazalishaji wadogo. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde alieleza kuwa Kiwanda cha kuzalisha chumvi cha STAMICO kipo hatua za mwisho, na kuagiza Shirika hilo kuhakikisha kabla ya mwezi wa Agosti kuisha kiwe kimekamilika na kuanza uzalishaji wa chumvi ili kupanua wigo wa soko la chumvi ya wazalishaji wadogo. Awali, akitoa taarifa ya utendaji wa Taasisi yao, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia aliishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto zilizokuwa zinaikabili sekta ndogo ya chumvi nchini ambazo zimepelekea bei ya chumvi kupanda na kuwanufaisha zaidi wazalisha chumvi nchini.