Serikali imepata jumla ya shilingi Trilion 1.877 kwenye sekta ya madini,mafuta na gesi

Serikali imepata jumla ya shilingi Trilion 1.877 kutoka kwenye kampuni 44 zilizolinganishwa katika Sekta ya Madini, mafuta na gesi ikiwa na tofauti ya kati ya malipo na mapato ya shilingi milioni 402.41 kwa mwaka kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa   wa Madini,  Anthony Mavunde katika uzinduzi wa ripoti ya 14 ya Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mavunde amesema kati ya kampuni hizo, kampuni 26 ni za Madini; Kampuni saba  ni za gesi asilia na mafuta; na Kampuni 11 ni kampuni zinazotoa huduma katika sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

Amesema,  kampuni zilionesha kuwa zililipa kiasi cha shilingi trillion  1.878 serikalini na kupelekea kuwepo na tofauti kati ya malipo na mapato ya shilingi milioni 402 sawa na asilimia asilimia 0.021 ya mapato yote yaliyoripotiwa na Serikali.

Aidha, Mavunde ameelekeza, tofauti hiyo sh milioni 402 kufanyiwa uchambuzi wa kina ili kujua visababishi vilivyosababisha kutofautiana ili Kamati iweze kuzipa makampuni na serikali

ushauri wa nini kifanyike ili tofauti hizo zisiendelee kujitokeza kwenye linganishi zitakazofuata.