Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze Septemba 9, 2024
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba nane za wakuu wa idara wa Halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani, zilizogharimu sh. milioni 960.5, Bashungwa ameielekeza TBA kuwa wabunifu katika kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za watumishi.Amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na TBA wafike Chalinze kujionea na kujifunza katika ujenzi wa nyumba zao za kisasa ili kupata mbinu bora za kuboresha na kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba hizo.
Aidha, Waziri Bashungwa amewataka watumishi kuwa wazalendo na kuacha urasimu wanapotoa huduma kwa wananchi .
Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa amezindua soko jipya la Chalinze lililogharimu sh. bilioni 1.7 na kuwashauri wajasiriamali kuwa wabunifu katika kuanzisha biashara tofauti ili waweze kupata soko kirahisi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Miundombinu cha Halmashauri ya Chalinze, Injinia Olais Sikoi, ujenzi wa nyumba nane za wakuu wa idara ulianza mwaka 2022 na kufikia asilimia 98 kukamilika.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
