WAZIRIΒ wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. AdolfΒ Mkenda akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 6,2024 jijini Dodoma kuhusuΒ kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Β linalofanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
WAZIRIΒ wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. AdolfΒ Mkenda,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa naΒ waandishi wa habariΒ kuhusuΒ kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Β linalofanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga, akizungumza na waandishi wa habariΒ kuhusuΒ kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na UbunifuΒ Β litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Katibu MkuuΒ Wizara yaΒ Elimu, Sayansi na TeknolojiaΒ Prof. CarolyneΒ Nombo,akielezea lengo laΒ kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na UbunifuΒ Β litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH ) Dkt.Amos Nungu,akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na UbunifuΒ Β litakalofanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Na.Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan kuzindua Mfuko wa Mikopo wa kusaidia Ubidhaishaji na Ubiasharishaji wa ubunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa Kitanzania.Β
Dkt.SamiaΒ anatarajia kufanya hayo akiwaΒ mgeni rasmi katika Kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu linalofanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 6,2024 jijini Dodoma Β amesema kongamano hilo linatarajia kufanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4, 2024Β katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam linalokwenda na Kauli mbiu ya Kongamano kwa mwaka huu kuwa niβMatumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ununifu katika Kuhimili Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi na Kuchangia kwenye Uchumi Shindaniβ.
Prof.MkendaΒ amesema Kongamano hiloΒ linalenga kuwaleta pamoja watafiti, wabunifu, na wadau kutoka sekta mbalimbali, ndani na nje ya nchi ili kujadili kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mchango wa Sayansi, teknolojia na ubunifu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Prof.Mkenda amesema kuwaΒ Rais Dk.SamiaΒ atazindua rasmi mfuko wa mikopo wenye kianzio cha Shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya kusaidia ubidhaishaji na ubiasharishaji wa bunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa Kitanzania;
“Katika Kongamano hilo Rais Dk.Samia atakabidhi hundi yenye thamani ya sh.bilioni 6.3 kwa watafiti 19 katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo nishati safi ya kupikia, atawatambua na kutoa tuzo maalumu kwa wanasayansi na wabunifu ambao matokeo ya kazi zao yamechangia kuleta mabadiliko ya kiuhumi na kijamii, ndani na nje ya nchi,”amesema Prof.Mkenda
Aidha amesema kuwaΒ kabla ya hafla ya ufunguzi,Β Rais SamiaΒ Β atapata fursa ya kutembelea maonesho ili kujionea baadhi ya matokeo ya utafiti na ubunifu ambayo yamechangia katika kubadili mfumo wa kiuchumi na kijamii hapa nchini.
Pia Prof.Mkenda amesema kuwaΒ kupitia Kongamano hilo Serikali itapata michango ya kisera na kitaalamu ambayo itasaidia kuimarisha sera, mikakati, na juhudi nyingine zinazolenga kuimarisha mchango na mshikamano baina ya taasisi, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo katika kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kama nyenzo kuu ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania.
Hata hivyo Prof.Mkenda,amewaalika Watanzania wote pamoja na wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi, ndani na nje ya nchi, kushiriki Kongamano hilo.
βili kufanikisha na kufikia malengo yaliyokusudiwa, nitumie fursa hii kuwaalika Watanzania wote pamoja na wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi, ndani na nje ya nchi, kushiriki Kongamano hili la STICE na hata wale watakaoshindwa kuhudhuria kwasababu tofauti tofauti wafuatulie kongamano hili kwenye luninga kwasababu litakuwa mubashara,
βUshiriki wenu ni muhimu sana katika kuleta mawazo na mikakati mipya, kuimarisha utafiti na ubunifu, na kuhakikisha kuwa matokeo ya utafiti na ubunifu yanajibu mahitaji na kutatua changamoto za maendeleo ya kiuchumi na kijamii,βamesema Prof.Mkenda.
Β
The post ππππ πππππ ππππππππ ππ πππ ππ ππππππππππ ππππ ππ πππππππ π appeared first on Mzalendo.