TTC Memphis yatinga nusu fainali tabora

 TTC Memphisi imekuwa ya kwanza kutinga nusu fainali ya Ligi ya Kikapu Tabora, baada ya kuvuna pointi 10 kutokana na ushindi wa michezo   mitano mfululizo. 

TTC inafuatiwa na Stylerz Centre yenye pointi nane na ingemaliza na tisa kama ingekamilisha  robo ya nne.

Kutokana na sheria ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu duniani (FIBA), timu inayofungwa inapata pointi moja na timu ikishinda inapata pointi mbili na katika mchezo huo Centre iligoma kumaliza robo ya nne

Nyingine ni Mboka Kings iliyopata pointi tano kutokana na michezo minne , huku Nzega Hawks  ikipata  nne kutokana na michezo mitatu.  

Urambo Sixiers ilipata  pointi nne kutokana na michezo minne, huku U.S.S Wolves  ikipata tatu  katika michezo mitatu.

Akiongea na Mwanasposti kwa simu kutoka Tabora, Mwenyekiti wa kamati na mashindano, Rorgers Kitenge alisema timu nne  zitakazoshika nafasi za juu zitacheza nusu fainali ya michezo mitatu ‘best of three play off’, na itayoshinda miwili itaingia fainali.