MATI FOUNDATION YAZINDULIWA RASMI NA DC BABATI .

Mwandishi Wetu ,Manyara.

Taasisi isiyokua kiserikali ya Mati Foundation yenye lengo la kusaidia jamii ,wahitaji na makundi maaalumu ikiwemo wenye ulemavu iliyoko chini ya kampuni ya Mati Super Brands Limited imezinduliwa rasmi leo na Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda katika makao makuu ya kampuni hiyo Mjini Babati mkoani Manyara..

Akizungumza mara baada ya kuzindua Taasisi ya Mati Foundation .Mkuu wa Wilaya ya Babati amempongeza Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd David Mulokozi kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayomzunguka katika Wilaya ya Babati na Tanzania kwa ujumla kwa kutoa sehemu ya faida anayoipata kusaidia jamii.

Emmanuela amesema kuwa kampuni hiyo imekua ikiunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kupitia misaada mbali mbali wanayoitoa kwa jamii ya Watanzania.

“Nipende kuipongeza Bodi ya Mati Super Brand Limited kwa kuja na wazo la kusaidia jamii kupitia Taasisi ya Mati Foundation na kuifikiria zaidi jamii ya Wananchi wa Babati na Tanzania kwa ujumla” Anaeleza Mkuu wa Wilaya ya Babati.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mati Foundation ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa ndoto yake ni kunyanyua jamii inayomzunguka kwa kurudisha sehemu ya faida anayoipata mwa jamii jambo ambalo limekua ni utamaduni wao na ibada pia.

“Tunapowasaidia watu tunafanya kwa Moyo na Upendo mkubwa na tunajitagidi mengi tunayafanya na hatuyasemi hadharani ,tumekua tukigusa watu mbalimbali na makundi mbali mbali” Anaeleza Mulokozi.

Mwenyekiti Msaidizi wa Mati Foundation Gwandumi Mpoma amesema kuwa tayari wametumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kusaidia jamii inayozunguka kama mchango wao kwa jamii tangu kiwanda hicho kilipoanzishwa mwaka 2017.

Mpoma amesema kuwa wamekua wakitoa misaada sehemu mbali mbali ikiwemo kwenye maaafa ya Mafuriko hanang,kusaidia fimbo nyeupe kwa wenye ulemavu wa macho pamoja na kutoa misaada kwa yatima,wajane na wazee.

Related Posts

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi ▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi ▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio ▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini Dar es Salaam Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo ikiwemo upunguzaji wa ada ya pango kwa mwaka ya leseni (Annual Rent) za uchimbaji mdogo wa chumvi nchini ili kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuchochea uzalishaji wa wingi wa chumvi nchini. Hayo yamesemwa jana tarehe 15 Julai, 2025 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Kikao cha wadau wa sekta ndogo ya chumvi chini ya Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA). "*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kutubeba sekta ya madini na wachimbaji kwa ujumla. Ni yeye aliyetuelekeza kusikilize kilio chenu na kutatua changamoto zinazowakabili ili mnufaike na shughuli mnazofanya" "Ametuelekeza Wizara ya Madini tuliridhie ombi lenu na kupunguza ada ya pango ya mwaka ya leseni ya uchimbaji mdogo kutoka Shilingi 45,000 mpaka Shilingi 20,000 kwa hekta, hili linakwenda kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ubora wa chumvi ya mzalishaji mdogo" alieleza Mhe. Mavunde. Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo udhibiti wa chumvi inayoingizwa kutoka nje ya nchi, zimepelekea bei ya chumvi ghafi kuongezeka na hivyo kuwanufaisha zaidi wazalishaji wadogo wa chumvi nchini. Uanzishwaji wa kodi ya zuio ya asilimia mbili (2%) kwenye mauzo ya chumvi ghafi kwa wazalishaji wenye leseni za PML imekuwa ni neema na manufaa kwao badala ya utaratibu wa awali wa kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato, ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wazalishaji wadogo. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde alieleza kuwa Kiwanda cha kuzalisha chumvi cha STAMICO kipo hatua za mwisho, na kuagiza Shirika hilo kuhakikisha kabla ya mwezi wa Agosti kuisha kiwe kimekamilika na kuanza uzalishaji wa chumvi ili kupanua wigo wa soko la chumvi ya wazalishaji wadogo. Awali, akitoa taarifa ya utendaji wa Taasisi yao, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia aliishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto zilizokuwa zinaikabili sekta ndogo ya chumvi nchini ambazo zimepelekea bei ya chumvi kupanda na kuwanufaisha zaidi wazalisha chumvi nchini.