Chadema yadai kukamata maboksi ya kura

 

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kimekamata karatasi za kura zilizopigia kura wagombea wa CCM kabla ya uchaguzi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa liyotolewa kwa umma na John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki , Mawasiliano na Mambo ya Nje amesema kuwa jimbo la Igunga mawakala wa Chama hicho wamekamata wamekama karatasi za kura zaidi ya 200 zilizopigia wagombea wa CCM,

Taarifa hiyo inasema kuwa Mawakala wa Chadema wa Kibaha vijijini katika Mtaa wa Kwa Mathias wamekamata masanduku yenye kura zilizopigwa lakini Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wamefika kwenye kituo husika na kuwatuhumu mawakala hao kuwa wameharibu uchaguzi na kuamua kuwakamata.

Kwenye Taarifa hiyo Mrema amesema kuwa jimbo la Chato katika kituo cha Nyantimba mawakala wa Chadema wamekamata maboksi sita ya kura ambazo zishapigwa kwa wagombea wa CCM hali hiyo imejitokeza na Jimbo la Bariadi

“Jimbo la Kilosa kijiji cha Dumila mpaka saa nne hii zoezi la kupiga kura halijaanza kwa sababu hakuna karatasi zenye nafasi ya mgombea wa kijiji. Hali hii inafanana na ile ya Jimbo la Msalala zoezi la kupiga kura limechelewa kwa sababu karatasi za kupiga kura zimechanganywa za kitongoji Isaka zimepelekwa Igudija”

About The Author