Alliance One Tobacco yashinda tuzo za ATE za mwajiri bora wa mwaka

KAMPUNI ya Tumbaku ya Alliance One Tanzania Limited(AOTTL) imeibuka mshindi wa jumla katika kuzalisha ajira nchini iliyotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania(ATE).

Kampuni hiyo yenye kiwanda cha tumbaku mjini Morogoro ilikabidhiwa tuzo ya ushindi huo mwishoni mwa wiki mkoani Dar es Salaam. 

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Meneja Rasilimaliwatu wa kampuni hiyo, Blasius Lupenza alisema kampuni hiyo inajivunia kuwa na usimamizi na uongozi mzuri pamoja na wafanyakazi wote kwa kusimamia sera za kampuni na utamaduni wa kufanya kazi. 

Alisema, “Kwa niaba ya kampuni tunajivunia sana kusherehekea mafanikio haya bora ya kuwa mshindi wa jumla na pia mshindi kwenye Kitengo cha kuzalisha ajira, kujitolea katika usimamizi wa wafanyakazi, bidi na ari ya ubunifu imeinua kampuni yetu kwenye ukurasa mpya”.

Aliongeza: “Tuzo hizi ni ushuhuda wa mchango wa kipekee na tunashukuru kuwa nao kama sehemu yetu. Tunashukuru ATE kwa kututia moyo”.

Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka imejikita katika kuangalia namna taasisi inavyofanya kazi kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo sayansi, taaluma, watendaji wa taasisi, usimamizi wa mashirika katika uwekezaji mdogo na wa kati. 

Kwa mwaka huu zaidi ya kampuni na taasisi 100 zilionesha nia ya kushiriki lakini ni 76 pekee zilichaguliwa katika kuwania tuzo hizo zilizogawanywa katika vipengele 10.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko amekipongeza ATE kwa kuandaa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka na kuwataka washindi kuzingatia viwango vitakavyofanikisha kuendeleza ubora mahali pa kazi.

Dk Biteko alisisitiza kuwa tuzo hizo zinahamasisha ushindani baina ya waajiri na kusaidia kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo usalama kazini, kuongeza viwango vya uzalishaji na kuboresha uhusiano mzuri na wafanyakazi kwa maendeleo ya kampuni na taasisi zao. 

“Ninawapongeza ATE kwa kuja na tuzo hizi zitakazosaidia kuboresha mazingira ya kazi na waajiri katika maeneo ya kazi, tunaamini tuzo hizi zitaendelea kuhamasisha ushindani kwa wafanyakazi ili kuendelea kuwa bora zaidi,” alisema. 

Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka ni moja ya mpango wa ATE unaofanyika kila mwaka tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 ambapo mwaka huu imetimiza miaka 19. 

Lengo la kutoa tuzo hizo ni kuhamasisha nguvu kazi ya pamoja na rasilimaliwatu ili kutekeleza majukumu ya msingi katika uzalishaji na utendeji katika biashara ndani ya kampuni.

Aidha ATE imelenga kuziwezesha taasisi kufanikiwa kutekeleza sera na mipango ya taasisi itakayosaidia kuongeza uzalishaji na ushindani wa kibiashara.

Ofisa Mtendaji mkuu wa ATE, Suzanne Ndomba alisema tuzo hizo zilianzishwa kwa lengo la kuwatambua waajiri wanaotekeleza mipango madhubuti inayosaidia kusimamia wafanyakazi na biashara kwa ujumla.

“Tangu kuanzishwa kwake tuzo hizi zimeendelea kuhasisha kampuni kuweka juhudi katika maeneo haya kwa kuzingatia sheria, kuweka sera, kanuni na mazingira rafiki ili kuongeza tija na ushindani,” alisema.Naibu Waziri Mkuu Mh.Doto Biteko, akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Alliance One Tobacco company ya Morogoro, Bw.Blasius Lupenza baada ya kampuni yake kuibuka mshindi wa jumla upande wa uzalishaji wa ajira katika tuzo za Mwajiri Bora zinazoratibiwa na Umoja wa Waajiri Nchini(ATE) zilizofanyika mwishoni mwa wiki.

Related Posts

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi ▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi ▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio ▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini Dar es Salaam Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo ikiwemo upunguzaji wa ada ya pango kwa mwaka ya leseni (Annual Rent) za uchimbaji mdogo wa chumvi nchini ili kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuchochea uzalishaji wa wingi wa chumvi nchini. Hayo yamesemwa jana tarehe 15 Julai, 2025 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Kikao cha wadau wa sekta ndogo ya chumvi chini ya Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA). "*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kutubeba sekta ya madini na wachimbaji kwa ujumla. Ni yeye aliyetuelekeza kusikilize kilio chenu na kutatua changamoto zinazowakabili ili mnufaike na shughuli mnazofanya" "Ametuelekeza Wizara ya Madini tuliridhie ombi lenu na kupunguza ada ya pango ya mwaka ya leseni ya uchimbaji mdogo kutoka Shilingi 45,000 mpaka Shilingi 20,000 kwa hekta, hili linakwenda kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ubora wa chumvi ya mzalishaji mdogo" alieleza Mhe. Mavunde. Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo udhibiti wa chumvi inayoingizwa kutoka nje ya nchi, zimepelekea bei ya chumvi ghafi kuongezeka na hivyo kuwanufaisha zaidi wazalishaji wadogo wa chumvi nchini. Uanzishwaji wa kodi ya zuio ya asilimia mbili (2%) kwenye mauzo ya chumvi ghafi kwa wazalishaji wenye leseni za PML imekuwa ni neema na manufaa kwao badala ya utaratibu wa awali wa kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato, ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wazalishaji wadogo. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde alieleza kuwa Kiwanda cha kuzalisha chumvi cha STAMICO kipo hatua za mwisho, na kuagiza Shirika hilo kuhakikisha kabla ya mwezi wa Agosti kuisha kiwe kimekamilika na kuanza uzalishaji wa chumvi ili kupanua wigo wa soko la chumvi ya wazalishaji wadogo. Awali, akitoa taarifa ya utendaji wa Taasisi yao, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia aliishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto zilizokuwa zinaikabili sekta ndogo ya chumvi nchini ambazo zimepelekea bei ya chumvi kupanda na kuwanufaisha zaidi wazalisha chumvi nchini.