KAYA 19,530 KUNUFAIKA NA MAJIKO YA GESI YA RUZUKU MKOANI ARUSHA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Musa akisisitiza jambo wakati wa utambulisho wa mradi wa usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya 50% mkoani humo. Mradi huo unasimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

………

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Lake Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 406.7 wa kusambaza majiko ya gesi 19,530 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% katika maeneo ya vijijini ndani ya Wilaya ya Arusha, Karatu, Longido, Meru, Monduli na Ngorongoro Mkoani Arusha.

Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya amebainisha hayo Desemba 6, 2024 Mkoani Arusha wakati wa kumtambulisha mtoa huduma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

“Tumeanza utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao unasisitiza miaka 10 kutoka sasa 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, na hili linaweza kufikiwa kupitia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo hii ya usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku,” alisema Mhandisi Yesaya.

Alifafanua kuwa REA imeandaa programu mbalimbali ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali ambayo imeasisiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya za wananchi wake sambamba na kuhifadhi mazingira kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za Nishati Safi ya kupikia ili kupunguza ukataji miti ambapo alibainisha kuwa takribani hekta 400,000 hukatwa kila mwaka.

“Mradi huu unakwenda kusaidia kuondokana na athari za kiafya, pia utasaidia kuepuka vitendo vya kikatili, kulinda vyanzo vya maji na kutunza Mazingira na pia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi,” alifafanua Mhandisi Yesaya.

Aidha, alisema kuwa mradi huo vilevile ni nyenzo muhimu ya kupunguza umaskini miongoni mwa jamii za maeneo ya vijijini kwani utatoa fursa kwa akina mama kujikita katika shughuli za uzalishaji mali pindi wanapotumia mitungi ya gesi kama njia mbadala ya kupikia sababu inaokoa muda ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Musa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango huo ambao amesema unakwenda kusaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kumudu gharama ya manunuzi ya majiko hayo ya gesi.

“Tunashukuru kwa mawazo haya ya Mhe. Rais na kwa kazi inayofanywa na REA. Ninaamini kwa ruzuku hii iliyowekwa na Serikali, Watanzania walio wengi wataweza kumudu gharama na hii itafanikisha lengo la 80% ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034,” alisema.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya Lake Gas, Kanda ya Kaskazini, Ismail Juma alithibitisha kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha wanufaika wa majiko hayo wanafikiwa kikamilifu na alitoa wito kwa wananchi mkoani humo kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Serikali kupitia REA.

Alitoa rai kwa wananchi kutumiza masharti ya kupata majiko hayo ya ruzuku ikiwa ni pamoja na kuwa na kitambulisho cha Taifa cha NIDA ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa kila mwananchi.

Wakala wa Nishati Vijijini unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.

Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya (kulia) akikabidhi taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku Mkoani Arusha kwa Katibu Tawala wa mkoa huo, Missaile Musa wakati wa kumtambulisha mtoa huduma anayesambaza majiko hayo mkoani humo.

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Musa akisisitiza jambo wakati wa utambulisho wa mradi wa usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya 50% mkoani humo. Mradi huo unasimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Related Posts

▪️Serikali kupunguza ada ya kodi ya pango kwa mwaka kwa Leseni ya chumvi ▪️Rais Samia apongezwa kwa kiwanda cha kusafisha chumvi Lindi ▪️Wazalishaji wa chumvi wafurahia kuanza kwa kodi ya zuio ▪️Serikali kudhibiti uingizaji wa chumvi kiholela nchini Dar es Salaam Katika kuwajengea uwezo wazalishaji wa chimvi nchini,Serikali imekuja na mikakati mbalimbali kufikia azma hiyo ikiwemo upunguzaji wa ada ya pango kwa mwaka ya leseni (Annual Rent) za uchimbaji mdogo wa chumvi nchini ili kusaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuchochea uzalishaji wa wingi wa chumvi nchini. Hayo yamesemwa jana tarehe 15 Julai, 2025 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Kikao cha wadau wa sekta ndogo ya chumvi chini ya Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA). "*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kutubeba sekta ya madini na wachimbaji kwa ujumla. Ni yeye aliyetuelekeza kusikilize kilio chenu na kutatua changamoto zinazowakabili ili mnufaike na shughuli mnazofanya" "Ametuelekeza Wizara ya Madini tuliridhie ombi lenu na kupunguza ada ya pango ya mwaka ya leseni ya uchimbaji mdogo kutoka Shilingi 45,000 mpaka Shilingi 20,000 kwa hekta, hili linakwenda kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ubora wa chumvi ya mzalishaji mdogo" alieleza Mhe. Mavunde. Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo udhibiti wa chumvi inayoingizwa kutoka nje ya nchi, zimepelekea bei ya chumvi ghafi kuongezeka na hivyo kuwanufaisha zaidi wazalishaji wadogo wa chumvi nchini. Uanzishwaji wa kodi ya zuio ya asilimia mbili (2%) kwenye mauzo ya chumvi ghafi kwa wazalishaji wenye leseni za PML imekuwa ni neema na manufaa kwao badala ya utaratibu wa awali wa kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato, ambao ulikuwa ni kero kubwa kwa wazalishaji wadogo. Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde alieleza kuwa Kiwanda cha kuzalisha chumvi cha STAMICO kipo hatua za mwisho, na kuagiza Shirika hilo kuhakikisha kabla ya mwezi wa Agosti kuisha kiwe kimekamilika na kuanza uzalishaji wa chumvi ili kupanua wigo wa soko la chumvi ya wazalishaji wadogo. Awali, akitoa taarifa ya utendaji wa Taasisi yao, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA), Bi. Hawa Ghasia aliishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto zilizokuwa zinaikabili sekta ndogo ya chumvi nchini ambazo zimepelekea bei ya chumvi kupanda na kuwanufaisha zaidi wazalisha chumvi nchini.