DRC Yaishtaki Rwanda Mahakama Ya Afrika – Global Publishers



Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imewasilisha kesi dhidi ya Rwanda katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu ICJ kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tuhuma za DRC dhidi ya Rwanda zinahusiana na mzozo uliokumba eneo la mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 2021, ambako vikosi vyake vimekuwa vikikabiliana na waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.

Kesi hiyoi itaanza kusikilizwa rasmi leo Jumatano ambapo hoja za pande hizo mbili kuhusu mamlaka ya mahakama hiyo na uwezo wake wa kusikiliza ombi iliyowasilishwa na DRC itasikilizwa.

Haya yanajiri siku chache baada ya Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, na Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, kukutana jijini Dar es Salaam Tanzania, kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo yenye makao yake jijini Arusha Tanzania, DRC  iliyosajili kesi hiyo mwaka 2023 inadai kuwa mzozo huo umesababisha mauaji, uvamizi wa maeneo yake, na watu 520,000 kulazimika kuyahama makazi yao, kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu na uharibifu wa shule na hivyo kusababisha watoto 20,000 kukosa elimu.

Aidha DRC inalalamikia uharibifu wa miundombinu mbinu yake kkama vile vifaa vya kusambaza umeme, uporaji na uharibifu wa miundombinu ya kilimo na vituo vya afya.