Afisa Mnadhimu namba Moja Mkoa wa Arusha ACP Debora Lukololo ambaye pia ni mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha TPF net amehudhuria Kikao kazi cha maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kikao hicho ambacho kiko chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa huo, Mheshimiwa Paul Christian Makonda.
Katika kikao hicho, wajumbe kutoka wizara mbalimbali, zikiwemo Wizara ya Michezo, Wizara ya Nishati, na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, wameshiriki kikao hicho kikiwa na lengo la kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mheshimiwa
Makonda amesisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha kuwa maadhimisho ya mwaka
huu yanakuwa yenye tija kwa wanawake wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.