Lissu afafanua maana ya No Refom No Election – Video – Global Publishers


Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu amefafanua kuhusu kauli mbiu ya chama hicho inayosema No Reform no electin alipozungumza na waandishi wa Habari kweye ofisi za chama hicho, Mikocheni jijini Dar es Salaam Amesema wao hawatatusia uchaguzi kama watu wanavyodhani lakini watafanya kila njia ili kubadili mfumo wa uchaguzi ambao unawapendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Tunaposema bila mabadiliko hakuna uchaguzi tuna maana gani? Tuna maaana kwamba kusipokuwa na mabadiliko yanayohitajika ya mfumo wa uchaguzi, tutafanya kila tunaloweza, kwa nguvu tulizonazo kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu haufanyiki mwaka huu” alisema Lissu.

Akaongeza: “ hatuzungumzii kususia uchaguzi, hatutasusia, tutaenda kuwaambia Watanzania, na tutaiambia jumuiya ya kimataifa, na tutawaambia walimwengu kwamba kama CCM na serikali yake haipo tayari kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi huru na za haki, uchaguzi wa mwaka huu usifanyike kabisa, ndiyo maana ya ‘No Reform No Election’ yaani bila mabadiliko hakuna uchaguzi.”alisema Lissu.

Akafafanua: “ Ninataka niwe wazi hapa, huu siyo uamuzi wa Mwenyekiti mpya wa Chadema Tundu Lissu, huu ni msimamo wa Chadema kama ulivyowekwa na vikao vyake vya juu vya kikatiba: Kamati Kuu, Baraza Kuu, na Mkutano Mkuu wa Taifa.”

Lissu alisema hawawezi kuachia mfumo huo ambao unasababisha wizi wa kura lakini pia mauaji kwa wapinzani akitoa mfano wa chaguzi zilizopita ambapo baadhi ya wapinzani waliuawa.

Amedai kwamba mfumo wa sasa wa uchaguzi unaipendelea CCM kwa sababu viongozi wote wa tume ya uchaguzi ni wateuliwa wa mwenyekiti wa CCM ambaye pia naye ni mgombea.

Stori na Elvan Stambuli | GPL