Serikali Imeombwa kupeleka Wataalam UDOM ili waweze kubobea katika Fani ya TEHAMA

 

Na Jane Edward, Arusha 

Serikali imeombwa kuwapeleka watalamu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)ili waweze kupata mafunzo ya ubobezi katika fani ya TEHAMA  ili kuweza kuboresha utendaji kazi wao na kuleta tija kwa Taifa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari Mkoani Arusha,Naibu Makamo Mkuu wa Chuo,Taaluma,Utafiti na mshauri elekezi katika Chuo Kikuu cha Dodoma Prof.Razack Lokina.

Amesema kuwa ,kutokana na  kamisheni ya TEHAMA  kuwa katika chuo hicho na kuweza kufanya vizuri katika tehama ni vyema serikali ikapeleka wataalumu wake kwenye chuo hicho ili waweze kupatiwa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambayo yatawapa ubobezi kwenye utendaji kazi.

Ameongeza kuwa, chuo hicho kimekuwa kikifuata maelekezo ya serikali katika kuhakikisha inawekeza zaidi kwenye maswala ya TEHAMA ili kuwezesha shughuli za kitaaluma na kitafiti hali ambayo imeleta mafanikio makubwa serikalini.

‘kutokana na jitihada hizo zote tunazofanya tumeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watalaamu mbalimbali na wanafunzi  ambao wamefanikiwa kupita kwenye chuo chetu na wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali’alisema.

Naye Mhadhiri wa chuo hicho ndaki ya sayansi za kopyuta na elimu angavu ,Salim Diwani amesema kuwa ,wao kama chuo wamefanikiwa kubuni application ya akilli bandia kwa matatizo ya uzazi na hatua za afya ya mtoto .

Salim amesema kuwa ,application hiyo  imetengenezwa kwa lengo la kusaidia wamama wajawazito kutatua changamoto watakazokuja kukutana nazo kulingana na hali ya kiafya waliyonayo wakati huo.

MWISHO…..

Related Posts