Mtoto Wa Elon Musk Azua Gumzo Mitandaoni – Global Publishers



Msanii wa muziki wa Kanada anayefanya shughuli zake Marekani, Grimes(Kushoto)kwenye picha ya patoja na Elon Musk(Kulia)

Msanii wa muziki wa Kanada anayefanya shughuli zake Marekani, Grimes, amemkosoa vikali aliyekuwa mpenzi wake na baba wa watoto wake watatu, Elon Musk, kwa kumpeleka hadharani mtoto wao wa miaka minne, Lil X, katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Ikulu ya Marekani mapema wiki hii.

Grimes alieleza masikitiko yake kuhusu ukosefu wa “heshima” katika siasa za Marekani, licha ya hofu yake ya “kufurushwa kabisa nchini humo.”
Musk na mtoto wake, ambaye jina lake kamili ni X AE A-XII, walivutia umakini wa wanahabari katika mkutano ulioitishwa na Rais Donald Trump kwa ajili ya kusaini agizo la kiutendaji linalolenga kupunguza urasimu wa serikali ya shirikisho.

Badala ya mkutano huo kujikita kwenye ajenda hiyo, tahadhari yote ilihamia kwa Musk na mtoto wake, hali iliyozua mjadala mkubwa.

Grimes, ambaye jina lake halisi ni Claire Boucher, hakuwa ametambua kwamba mtoto wao alikuwa ameonekana hadharani katika Ikulu ya Marekani hadi alipofahamishwa kupitia mitandao ya kijamii. Baada ya kupata taarifa hizo, alitoa maoni yake kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), ambao Musk alinunua na kuupa jina la mtoto wao.

“Mtoto hapaswi kuwa hadharani hivi,” aliandika Grimes. “Sikuwa nimeona hili, asante kwa kuniarifu. Lakini ninafurahi kwamba alikuwa na adabu.”
Msanii huyo pia alieleza tahadhari yake kuhusu nafasi ya Musk inayozidi kuongezeka katika duru za kisiasa Marekani. Aliongeza kuwa hatua ya Musk kumweka hadharani mtoto wao ilikuwa “janga binafsi” kwake.


Related Posts