Kanisa La Nabii Suguye Latimiza Miaka 18 – Global Publishers

Kanisa la WRM Ministries lililo chini ya @prophet_nicolaus_suguye leo linatimiza Miaka18 tangu kuanzishwa kwake huku Prophet Nicholas Suguye akijivunia makubwa ambayo yametendwa na MUNGU kupitia WRM kwa waumini wake.

Kanisa limefanya mengi ikiwemo kusaidia Wajane,wazee na watoto yatima,pia wamefanya juhudi mbalimbali katika kuboresha Miundombinu ya barabara ambapo walichagiza kufanywa maboresho ya barabara ya kivule na baadae Serikali ikawasaidia kuiweka lami. Nabii Nicolaus Suguye ndiye Mwanzilishi na Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Neno la Upatanisho (The Word of Reconciliation Ministries – WRM), ambayo iko Matembele ya Pili, Kivule, Ukonga, katika Jiji la Dar es Salaam, Tanzania.

Nabii Suguye alizaliwa Kongowe, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Tanzania Bara. Amehudumu kama mhubiri wa Injili tangu mwaka 1998, na mwaka 2007 alianzisha Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM) jijini Dar es Salaam. Nabii Nicolaus Suguye amewasaidia wengi kuishi maisha ya ushindi kwa neno la Mungu. Kupitia ibada zake za miujiza, matangazo ya redio, vipindi vya televisheni, na mtandao wa intaneti, ujumbe wake usioyumba wa upendo wa Mungu umewahamasisha mamilioni ya watu kuanzisha uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Anajulikana kwa uwezo wake wa kinabii wa kunena Neno la Bwana kwa usahihi na wepesi mkubwa.

Anaendelea kujitoa kwa dhati zaidi kuliko hapo awali katika kuhubiri Injili ya Yesu Kristo, kufundisha Neno la Mungu lisilobadilika, na kutarajia nguvu kuu za Roho Mtakatifu zenye miujiza. Hivi leo, anafikia mamilioni ya watu kila siku kupitia teknolojia za kisasa, ikiwemo mitandao mbalimbali ya kijamii.

#Happy18AnniversaryWRM
Na Elvan Stambuli GPL