Aliyekamatwa Ni Kishandu – Global Publishers



Jeshi la Polisi limetoa taarifa kwa umma kuhusu video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha mwanaume mmoja akikamatwa kwa nguvu.

Taarifa ya polisi imeeleza kwamba aliyekamatwa ni Rajabu Hassan ambaye anatuhumiwa kwa matukio kadhaa ya uporaji wa kutumia pikipiki maarufu kama vishandu.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba mtuhumiwa alikuwa akitafutwa na polisi ambapo walipojaribu kumkamata katika eneo la Mwendapole, aliwakimbia polisi akiwa anaendesha pikipiki isiyokuwa na plate number.

Inazidi kuelezwa kuwa katika tukio hilo lililotokea Februari 20, 2025 katika eneo la Maili Moja, Pwani, mtuhumiwa huyo alianzisha vurugu licha ya polisi kujitambulisha ambapo polisi walifanikiwa kumkamata na kumpeleka Kituo cha Polisi Kibaha ambapo ndugu zake wanazo taarifa za kukamatwa kwake.