Mwanasiasa mkongwe nchini aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya mkoani Mara na aliyewahi kuwa waziri kwenye wizara mbalimbali, Profesa Philemon Sarungi amefariki dunia Machi 5, 2025 jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa marehemu, Maria Sarungi amethibitisha taarifa hizo, msiba upo nyumbani Oysterbay Mtaa wa Msasani Dar es salaam”
Profesa Sarungi alizaliwa Machi 23, 1936.
“Taarifa na taratibu nyingine zitatolewa na Familia, apumzike kwa amani Mzee wetu”