Wananchi wa Arusha Ni Mwendo Wa Kula Nyama Bure leo – Global Publishers



 

Vijana wajasiriamali wanaojishughulisha na uchomaji wa nyama Mkoani Arusha wameeleza kuendelea vyema na maandalizi ya Usiku wa nyama Choma jijini Arusha ambapo kufikia majira ya saa tano asubuhi leo Machi 07, 2025, tayari uchomaji wa nyama ulikuwa umeshaanza.

Kulingana na ratiba iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Paul Christian Makonda, ulaji wa nyama choma hiyo utaanza majira ya saa kumi na mbili za jioni, ukitanguliwa na futari ndogo iliyoandaliwa mahususi kwaajili ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo ambao wapo kwenye mfungo wa Ramadhan na Kwaresma.

 

 

Wananchi wa Arusha na wageni mbalimbali waliofika Mkoani hapa kwaajili ya shughuli za utalii pamoja na kilele cha siku ya wanawake hapo kesho Machi 08, 2025 watapata fursa ya kufurahia burudani ya muziki pamoja na ulaji wa nyama choma ambapo ng’ombe zaidi ya 400 wameandaliwa kwaajili ya shughuli hiyo sambamba na nyamapori ikiwemo ya pofu, nyati, nyumbu pamoja na swala, vyote vikiandaliwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia nishati safi katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kuzuia matumizi ya nishati chafu ya mkaa na kuni.