MRADI WA BIODIVERSITY FINANCE INITIATIVE WAZINDULIWA RASMI TANZANIA

 


Wadau mbalimbali wa maendeleo Nchini Tanzania wamekutana
jijini dar es salaam kama sehemu ya kujadili maswala mbalimbali yanayohusu
utunzaji wa viumbe hai kupitia Mradi wa Biodiversity finance initiative
uliozinduliwa jijini Dar es salaam na naibu katibu Mkuu ofisi ya makamu wa
Rais Mh. HASSAN MOHAMED HASSAN

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, ABDALLAH HASSAN
MITAWI amesema mabadiliko ya tabianchi yana mchango mkubwa katika kuathiri
viumbe hai na Mazingira nchini Tanzania ameyasema hayo katika uzinduzi wa Mradi
wa Biodiversity finance initiative ululiozinduliwa kwa mara ya kwanza Tanzania
Bara

 

 

Kwa upande mwingine mchambuzi wa programu wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) FERISTER IGNATUS amepongeza dhamira ya
Tanzania Bara katika kuunga mkono mpango wa kudhithibi uwepo wa viumbe hai na
Mazingira salama kwa jamii

 

 

HASSAN MOHAMED HASSAN ambaye ni mratibu wa BIOFIN Zanzibar
ameeleza sababu zinazopelekea Zanzibar kupata mafanikio katika mipango ya
kutunza Viumbe hai kupitia Mradi wa Biodiversity finance initiative ambapo sera
wezeshi na usimamizi mzuri zinatajwa kuwa sababu kuu za kufanikiwa kwa Mradi
huu

 

 

Mradi wa Biodiversity finance initiative unatajwa kuleta
mageuzi Tanzania Bara mara baada ya kuzinduliwa kwa mara ya kwanza huku wadau
mbalimbali wa maendeleo wakiunga mkono sera ya utunzaji viumbe hai

Related Posts