Rais Samia Alivyozindua majengo ya Mahakama ya Tanzania Dodoma (Picha +Video) – Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Majaji, Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Makazi ya Majaji Jijini Dodoma tarehe 05 Aprili, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Aprili 5, 2025 amezindua rasmi majengo ya Mahakama ya Tanzania kwa kukata utepe na kuweka jiwe la msingi katika moja ya majengo hayo, likiwemo Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania lililopo jijini Dodoma.

Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika kuboresha miundombinu ya utoaji haki nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema amefurahishwa na jinsi jengo la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma lilivyojengwa kwa kuzingatia ujumuishi wa makundi yote katika jamii.

Amesema ameona jinsi vyumba maalum vya watoto vilivyojengwa kwa namna ya kuwaondolea hofu kabla ya kutoa ushahidi au kuhojiwa.

Rais Samia akizindua Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Nyumba za Makazi ya Majaji Mkoani Dodoma, tarehe 05 Aprili, 2025.
Rais Dkt. Samia  akimkabidhi Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma mfano wa ufunguo mara baada ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Makazi ya Majaji tarehe 05 Aprili, 2025, Jijini Dodoma.