ACHANA na msimamo ulivyo wa Ligi ya Wanawake, JKT Queens ikiwa kileleni na pointi 38, timu hiyo inaongoza kwa kutoa vichapo kama ilivyo kauli mbiu yao ‘Kichapo cha Kizalendo’.
Msimu huu imetoa vipigo vitanpo hadi sasa sawa na ilivyotoa msimu uliopita wote na tayari imefunga mabao 56 ikiwa timu pekee iliyofunga mabao kuanzia 50 kwenye mechi 14, huku Simba ikiweka kambani 46 tofauti ya mabao 10.
Msimu huu timu hiyo ikiwa kwenye mbio za ubingwa imezifunga baadhi ya timu mabao kuanzia mabao matano na kuendelea kama ilivyokuwa msimu wa kwanz