BAADA ya Simba kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa timu hiyo umebainisha kuwa malengo makubwa ni kutwaa ubingwa.
Ni Aprili 20 Simba inatarajiwa kucheza na Stellenbosch FC ya Afrika Kusini mchezo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na nusu fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa Aprili 27 nchini Afrika Kusini.
Try Again, Mjumbe wa Kamati ya Klabu ya Simba ameweka wazi kuwa nia kubwa ni kuhakikisha wanachukua kombe hilo.
“Malengo yetu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa wa Afrika, Wanasimba wetu wote wanafuraha baada ya ushindi hivyo huu ni ushindi wa Wanasimba wote na Watanzania wote.
“Wachezaji tuliwaambia kwamba hii ni mechi kubwa wanapaswa kuwa katika upambanaji, kwanza tunakwenda kukaa chini kuangalia namna gani tutafika fainali.”
Simba ilipata ushindi Aprili 9 2025 kwa penalti 4-1 ikiwafungashia virago Al Masry kutoka Misri baada ya dakika 90 kusoma Simba 2-0 Al Masry ile robo fainali ya kwanza ugenini ilikuwa Al Masry 2-0 Simba.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.