Mwanamitindo maarufu na mke wa nyota wa klabu ya Yanga, Stephane Aziz Ki, Hamisa Mobetto, amejiunga rasmi na orodha ya wake na wapenzi wa wachezaji wa soka (WAGs) wanaopata kipato kikubwa zaidi kupitia machapisho ya kudhaminiwa kwenye Instagram kwa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mobetto hupokea kiasi cha dola 64,700 kwa kila chapisho la kibiashara analoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, sawa na takriban shilingi milioni 172.3 za Kitanzania.
Katika nafasi ya kwanza ya orodha hiyo yupo Georgina Rodriguez, mpenzi wa nyota wa soka duniani Cristiano Ronaldo, ambaye hupokea dola 236,900 kwa kila chapisho linalodhaminiwa — sawa na takriban shilingi milioni 638 za Kitanzania.
Antonela Roccuzzo, mke wa Lionel Messi, amepanda hadi nafasi ya pili kufuatia kuondoka kwa Anitta kutoka kwenye orodha hiyo.
Pamoja na Antonela, mastaa wengine wanaopata zaidi ya dola 130,000 kwa kila chapisho ni Becky G na Victoria Beckham, ambao nao ni wake wa wanasoka mashuhuri.