Heche adakwa na Polisi Kariakoo, apelekwa Central

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, John Heche, amekamatwa na Jeshi la Polisi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Kariakoo jirani na soko jipya la vyakula.

Kwa wa taarifa ilizopata Mwananchi jioni hii ya leo Jumanne Aprili 22, 2025 kutokea eneo la tukio, baada ya kuanza kuhutubia kwa takriban dakika tano, Polisi walifika na kumtaka aache kuhutubia, ndipo ikatokea vuta nikuvute kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema iliyodumu kwa dakika 30, hata hivyo wafuasi wa chama hicho walisema kama Polisi wanamuhitaji, watampeleka wenyewe kituoni. 

Hata hivyo, Heche alichukuliwa na wafuasi wa Chadema na kuelekea naye Kituo cha Polisi Msimbazi alikokaa kwa muda mfupi kabla ya kuchukuliwa gari la Jeshi la Polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi akiwa ameambatana na baadhi ya wafuasi wa chama hicho.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts