Rais Samia awapa magari ya kisasa Polisi, IGP Wambura asema…

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Camillus Wambura amemshukuru Amri Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa magari ya mapya na ya kisasa kwa ajili ya matumizi ya  operesheni mbalimbali za jeshi hilo.

IGP Wambura amesema hayo leo Jumatatu, Aprili 28,2025 jijini Dar es Salaam alipofanya ukaguzi wa magari hayo ambapo amesema yatarahisisha utendaji kazi wa jeshi hilo.

IGP Wambura amewasisitiza kuendelea kufanyakazi kwa utii, bidii, weledi na uadilifu huku akitoa shukurani kwa Rais Samia kwa maboresho makubwa aliyofanya kwa Jeshi la Polisi tangu alipoingia madarakani na kulifanya kuwa Jeshi la kisasa na lenye weledi mkubwa katika kutekeleza majukumu yake ya kazi za kila siku.

Related Posts