KATIBU MKUU KIONGOZI AZINDUWA MWEZI WA ELIMU KWA SHUNGULI ZA WAKAGUZI WA NDANI

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Dkt. Moses Kusiluka, akizungumza na maafisa wa Taasisi za Umma na Binafsi kwenye kikao cha mwezi kilichofanika jijini Dodoma Mei 2, 2025.

RAIS wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dk. Zelia Njeza (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka baada ya kufungua Mkutano wa Mwezi wa Ukaguzi wa Ndani uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma jana. Kulia ni Mkaguzi Mkuu wa ndani, Benjamin Magai.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka ametoa wito
kwa taasisis za Umma na Binafsi 
kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuwaamini wakaguzi wa ndani ili
kusadia kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kwa lengo la kusaidia kupunguza makosa yanayosababisha hati chafu na badala yake kuleta maendeleo chanya  katika taasisi na Taifa kwa Ujumla.

Balazi Dkt.KUSILUKA ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye
kikao cha mwezi cha maaafisa ukaguzi wa ndani ambapo amesema ni muhimu kufanya
kazi kwa kuzingatia welezdi na kufanya kazi kwa uwazi ili kufanikisha malengo
ya taasisi na Taifa.

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya wakaguzi wa Ndani
Tanzania (IIA) DKT. ZELIA NJEZA ameziomba 
taasisi za Umma na Binafsi Nchini 
kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa ndani ili wasaidie kuwapa Elimu juu
uendeshaji wa  taasisi hizo ili zifanye
kazi kwenye mlengo sahihi.

Related Posts