Azam FC yashtukia kitu kwa Nizar

WAKATI ikielezwa kuwa, Yanga iko katika mazungumzo na nyota wa JKU, Abubakar Nizar Othman, mabosi wa Azam FC wameweka wazi nyota huyo ni mali yao na hauzwi, hivyo wanaomtaka wasahau kuhusiana na hilo na mwishoni wa msimu huu watamrudisha.

Ipo Hivi. Mara baada ya mechi ya fainali ya Kombe la Muungano, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Gombani na Yanga kubeba taji kwa kuifunga JKU kwa bao 1-0, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said alionekana akizungumza na mchezaji huyo kwa muda mrefu uwanjani hapo.

Nizar aliyecheza beki wa kulia, licha ya kuwa kwa asili ni kiungo mkabaji, aling’ara kutokana na kuwa mtulivu, makini na mwenye uwezo mkubwa wa kusoma mchezo. Mazungumzo yake na Hersi yaliibua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka waliokuwa uwanjani hapo.

Related Posts