Dabi ya Kariakoo yapelekwa mkutano mkuu Yanga

BAADHI ya wanachama wa Klabu ya Yanga wamefikia hatua ya kuiandikia barua Kamati ya Utendaji kuomba kufanyika mkutano mkuu wa dharura kabla ya Juni 15, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Yanga, ili kuitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura inategemea idadi ya wajumbe waliopo na ridhaa ya kamati ya utendaji ya klabu au kwa shinikizo la wanachama.

Lakini, Katiba imeelekeza kwamba mkutano mkuu ili ufanyike inalazimu wanachama watano wa klabu hiyo kutoka kila tawi wahudhurie ambao ni wajumbe.

Kwa mujibu wa wanachama hao ambao ni viongozi wa matawi ya Yanga mkutano huo mkuu wanataka ajenda kuu iwe kujadili mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba ulioahirishwa Machi 8, 2025

Related Posts