Dar es Salaam. Treni ya abiria katika jiji la Dar es Salaam, inayofanya safari zake kati ya Kariakoo na Pugu, imepata ajali huku sababu ikitajwa kuwa ni mabehewa matatu kuacha njia.
Katika ajali hiyo, watu saba walijeruhiwa na kupelekwa hospitali ya Amana, hata hivyo walipata msaada wa haraka kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Mei 13, 2025, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, Peter Mabusi amesema ajali hiyo imetokea leo saa 11 jioni kati ya eneo la Kamata ikielekea Machinga Complex.
โNi kweli ajali hiyo imetokea leo saa 11 jioni wakati treni hiyo ikiwa inaelekea Pugu, na ni baada ya mabehewa matatu katika treni hiyo kuacha njia.
โHata hivyo, tunashukuru hakuna behewa lililoanguka zaidi ya kuinama na tayari waliokuwa ndani ya treni hiyo wameokolewa wakiwemo majeruhi saba,โ amesema Kamanda Mabusi.
Amesema wanashukuru waliwahi mapema katika eneo hilo la ajali na kuwaokoa majeruhi hao na kwa kuwa hakukuwa na purukushani, waliokuwa kwenye mabehewa mengine walitoka salama.
Endelea kutufuatilia Mwananchi