Licha ya mvua, mamia wajitokeza kuuaga mwili wa Charles Hilary

Licha ya mvua kubwa kunyesha katika mji Unguja, Zanzibar wananchi na viongozi kutoka maeneo mbalimbali wamefika Kisonge kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, ambapo zoezi hilo litaongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar, Charles Hilary alifariki dunia alfajiri ya Mei 11 katika Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu

Charles kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo Desemba 30, 2021, kisha kuteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Februari 6, 2023 alikuwa mtangazaji wa vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.

Related Posts