Boni Yai Anatoa Tamko, Kinachoendelea Chadema, Kujivua Uanachama Wake – Global Publishers



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Boniface Jacob.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, Boniface Jacob, leo Mei 18, 2025 amesema kuwa wakati na baada ya mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho, kulikuwapo na makundi tofauti ndani ya chama yaliyomuunga mkono kiongozi wao, jambo lililopelekea migogoro midogo ya maneno baina ya wafuasi wa wagombea tofauti.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari katika makao makuu ya CHADEMA Mikocheni, Boniface Jacob alibainisha kuwa baadhi ya watu waliounga mkono Mwenyekiti wa sasa, Tundu Lissu, walikuwa wakimtukana mwenyekiti mstaafu, Freeman Mbowe, na wale waliounga mkono Mbowe walifanya vivyo hivyo.

“Hali kama hii haimaanishi kuwepo kwa chuki kati yetu,” alisema Boniface, “hii ilikuwa sehemu ya ushindani wa uchaguzi ambapo kila upande ulikuwa na msimamo wake. Ukweli huu hauwezi kufichwa, lakini ni muhimu kuelewa kuwa tunapaswa kuendelea kuungana na kushirikiana baada ya uchaguzi.”

 











Related Posts