Chaumma yawateua Mrema, Ruge kuwa wakurugenzi wa habari na uchumi

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) imefanya uteuzi wa wakurugenzi wa idara mbalimbali ya chama hicho akiwemo John Mrema kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Taarifa kwa Umma.

Mrema atasaidiwa na Ipyana Samsom ambaye awali alikuwa akiiongoza Idara hiyo.

Aidha, Catherine Ruge ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchumi, Fedha na Mipango.

Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa Chaumma, Salum Mwalimu baada ya kumalizika kikao hicho kilichofanyika leo Jumamosi Mei 24, 2025 jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Hashim Rungwe.

Mwalimu amesema walioteuliwa wana uzoefu mkubwa kwenye maeneo yao hivyo hana shaka watatumika vilivyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts