Samia: Ilani mpya ya CCM itakuwa na mambo mazuri

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema chama hicho kitaiweka hadharani Ilani yake mpya ya 2025-2030 ambayo itanadiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025.

Samia amesema kuwa Ilani hiyo itazinduliwa kesho Ijumaa, Mei 30,2025 na kwamba, itasheheni mambo mazuri kwa maendeleo ya Watanzania.

Ameyasema hayo leo Alhamisi, Mei 29, 2025, wakati akifungua  Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ambapo amesema ilani hiyo imeandaliwa kwa weledi mkubwa na imewashirikisha wadau mbalimbali.

“Ilani ya uchaguzi mkuu wa 2025 inaakisi kipindi cha pili na cha mwisho cha utekelezaji wa sera za CCM kwa miaka 2025 hadi 2030. Tumeona ni muhimu kabla hatujaifikisha kwa wananchi tufanye mapitio ya ilani iliyopita ya mwaka 2020-2025 na ndiyo kazi tuliyoifanya leo,” amesema Samia.

Ameongeza kuwa matarajio yake ni kuona wajumbe wa mkutano huo wakibeba jukumu la kuisambaza ilani hiyo kwa wananchi pale utakapowadia wakati rasmi wa kampeni.
Imeandikwa na Faraja Masinde

Related Posts