Samia awatega wanachama wanaotamani kukipasua CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ni kama amewatega wana-CCM wanaowaza kukigawa chama hicho, akiwataka wajitafakari kwa kina kabla ya kufikia maamuzi hayo.

Akizungumza leo Alhamisi Mei 29, 2025 katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika jijini Dodoma, Rais Samia alitoa kauli hiyo baada ya kuoneshwa picha mnjongeo ya ramani ya jengo jipya la makao makuu ya chama hicho litakalogharimu Sh34 bilioni.

“Baada ya kuwa na jumba kama lile, heshima ile, wewe kama mwana-CCM, jiulize moyoni kwako, kweli unadhamira na moyo wa kupasua chama kama hiki? Tukishafika hatua kama ile kweli utashawishika kupasua chama hiki? Sasa hilo ni assignment (kazi) kila mtu akae ajiulize mwenyewe, CCM oyeee,” amesema Rais Samia.

Amesisitiza kuwa pindi litakapokamilika jengo hilo ni ishara ya ukuaji na uimara wa chama, akiwataka wanachama wote kushirikiana katika kulitumikia kwa umoja badala ya kulipasua.

Related Posts