Dar es Salaam. Kufuatia malalamiko ya wananchi wa Mbopo kata ya Mbwepande, kudai kuwa Shirika la Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam (DDC) linataka kuwapora maeneo yao, Mkuu wa Wilaya ya Kinondo-ni, Saad Mtambule amesema hakuna mwananchi atakayeondolewa kwenye eneo lake.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka wanan-chi hao kukubali ukweli eneo wanalokaa ni la DDC na walipie kiwango cha fedha wali-choridhia kwenye mikutano waliyokaa kipindi cha nyuma, jambo ambalo baadhi ya wananchi walikataa.
Sababu ya wananchi hao kugoma kulipia ni madai kuwa eneo wanaloishi sasa, pamoja na kwamba DDC inadai ni lao, tayari wananchi wameliendeleza tangu likiwa pori na hawakuwahi kumuona mamlaka yoyote mtu iliyowafuta kueleza inamiliki eneo hilo.
“Maelekezo ya Serikali ni kutoleta taharuki na watu wasiondolewe kwenye haya mae-neo, tumesimamia hilo kwa kuwa hili ni eneo la DDC na tunajua kwamba wananchi wamenunua haya maeneo.
“Wapo matapeli kwenye haya maeneo tutahakikisha utaratibu mzuri unawekwa kiserikali, hasa kulipa Sh3,000 kwa mita za mraba kwa utaratibu ambao mlikubaliana kwenye kikao,” amesema.

Mtambule amesema watawasiliana na Wa-ziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na viongozi wengine kufika mtaa wa Mbopo kuendelea kutatua migo-goro hiyo.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi hao kuondoa dhana ya kuamini kwamba DDC hawakuwahi kuwepo kwenye eneo la Mbopo.
“Nimekuja 2023, DDC nimeikuta na maele-zo hayo yalikuwepo, kwa hiyo nashauri tusirudi nyuma kusema kwamba DDC hakuwepo.
DDC alikuwepo na maeneo haya yalikuwa mapori, huu ndio ukweli mchungu ambao hamtaki kuamini,” amesema.
Awali, wananchi hao walipowasilisha kero zao kwa mkuu huyo wa wilaya, mkazi wa mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Beda Mchomba amesema yupo Mbopo tangu mwaka 1995 na wao ndio walioondoa vi-chaka.
“Sisi hatupo tayari kulipia Sh3,000 na eneo DDC wakilipima kipande changu kisiende kwa mtu mwingine,” amesema.
Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Christina alisema yeye ni mi-ongoni mwa wananchi ambao eneo lake lil-ipimwa na DDC na kipande kilichobaki kupewa jirani yake.
Hoja ya mwananchi huyo ni kwanini se-hemu ya eneo lake aongezewe mtu mwingine wa jirani, akitafsiri hali hiyo kuwa ni kuwatengenezea migogoro.
Hoja nyingine iliibuliwa na Elinoela ali-yesema kila mwaka analipia eneo lake kodi ya ardhi na ana hati, lakini anaambiwa eneo lake alinunue kwa mfumo mpya am-bao tayari umewekwa.
“Kila mwaka nalipa kodi, sasa inakuaje eneo langu linauzwa na hati yangu niliyo-nayo ipo hai, lakini walioweka kwenye mfumo hati yangu haipo tena,” amesema.
Kilio hicho kinafanana na cha Magu Mtem-be, ambaye alilalamika mwaka 2014 alin-unua ardhi eneo la Mbopo kwa Sh35 mil-ioni na kupewa mkataba wa kisheria, lakini anaambiwa eneo hilo si lake na tayari lime-anza kupimwa na DDC.
Jambo analodai kumshangaza ni kwamba katika eneo lake alikata kipande na ku-muuzia mtu mwingine ambaye alianza ku-jenga, na eneo la mtu huyo likatambuliwa kuwa lake, lakini yeye, kutokana na kuto-kuliendeleza eneo lake, limewekwa kwenye mfumo wa Serikali na anapaswa kulilipia tena.
“Juzi nimekopa Sh20 milioni na nikajenga vibanda kwenye eneo hilo na hadi sasa nimewekeza Sh50 milioni kwenye eneo langu,” amesema.
Naye Beatrice Elisha alilalamika kuwa eneo lake alilinunua mwaka 2020, lakini sasa anaambiwa ni mvamizi wa eneo hilo, ameomba Serikali iweke utambulisho wa kila eneo ili kuepusha wananchi kuvamia na kuleta migogoro.
“DDC inapokuja kuweka alama kwenye maeneo, elimu hatujapewa,kwa hiyo ni muhimu Serikali isitishe utaratibu huu hadi mgogoro huu utatuliwe,” amesema.
Akizungumzia kinachofanywa na DDC kwenye maeneo hayo, Mtambule ames-ema lengo la Serikali si kuwanyanyasa wananchi, bali kinachofanyika ni kuyapan-ga maeneo hayo.
“Ili kupangwa, lazima kuwe na barabara na huduma za kijamii, hili ndilo lengo namba moja, pia wapo wananchi wanalalamika kwamba hawajashirikishwa.
Kama hakukuwepo ushirikishwaji kama wananchi wanavyosema, hilo si jambo je-ma hata kidogo,” amesema.
Mtambule amesema kwa kuwa mradi huo ni wa Serikali, ulipaswa wananchi washiri-kishwe hatua kwa hatua.
“Kitu kingine ambacho kimenishtua ni mtu kukatwa eneo lake au kuuzwa lote,hili si-wezi kulitolea majibu sasa, nitakwenda kufuatilia ukweli wake,” amesema.
Mkuu huyo wa wilaya alihitimisha kwa ku-wataka wananchi hao, kwa kuwa kero zao zinatofautiana, waandikishe majina yao na kero walizonazo pamoja na kuambatanisha hati zao ofisi ya mtendaji.
Amesema Jumatatu atatembelea maeneo yote ambayo wananchi wataorodhesha kwa mtendaji .
Ikiwa ni hatua ya kutafuta suluhu zaidi ya mgogoro huo Mei 29,2025 Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee ‘aliwaka’ bungeni akitaka Serikali ieleze hatima ya wananchi wa mitaa saba katika majimbo ya Kawe na Kibamba jijini Dar es Salaam.
Mdee ametoa kauli hiyo bungeni jijini Do-doma leo Alhamisi Mei 29, 2025 wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2025/26.
Hata hivyo, Waziri wa Wizara hiyo, Deo Ndejembi amekiri kuwepo kwa migogoro hiyo lakini akasema tayari walishakaa na wahusika katika eneo hilo ambalo lina nyumba zaidi ya 200,000 na tayari mipan-go mizuri inaendelea.
Katika mchango wake, Mdee ame-zungumzia usumbufu na adha wanayoku-tana nayo wananchi wa mitaa ya Mabwe-pande, Mbopo na Madale katika jimbo la Kawe na wale wa Tegeta A, Msumi A, Msumi B na Kulangwa ambayo jimbo la Kibamba akisema wapo kihalali lakini wanaonewa.
Amesema Ndejembi ni waziri wa tatu kutaka kusikiliza mgogoro huo ambao mara ya kwanza alikuwepo Waziri Angelina Mabula kisha Jerry Silaa lakini wote ha-wakufikia mwisho ndiyo akamuomba ajita-hidi kuumaliza ili wananchi wapate haki yao.