Ilani mpya ya CCM yabeba vipaumbele tisa

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Profesa Kitila Mkumbo amesema ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2025/2030 imebeba vipaum-bele tisa ikiwemo kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii.

Vipaumbele vingine ni kuchochea mapinduzi ya kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uli-ojengwa katika msingi wa kuongeza thamani rasilimali zinazozalishwa nchini na kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuongeza kipato kwa wananchi na kupunguza umasikini.

Profesa Kitila amebainisha hayo leo Ijumaa Mei 30, 2025 wakati akiwasilisha Ilani muhtasari wa ilani hiyo katika mkutano mkuu maalumu wa CCM unaondelea jijini Dodoma.

Mwenyekiti huyo alitaja vipaumbele vingine kuwa ni kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirfishaji, kukuza na kuimarisha matumizi ya sayansi na takenolojia ya sayansi na teknolojia.

“Kudumisha demokrasia na utawala bora, kuendelea kudumisha amani, utulivu na usalama na kudumisha utamaduni wa Taifa, kukuza, sanaa na michezo na kuongeza kasi ya maendeleo viji-jini,” amesema Profesa Kitila.

Kuhusu kipaumbele cha kuongeza kasi ya maendeleo vijijini, Profesa Kitila alimweleza Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan kuwa: “Hili ni eneo jipya katika miaka mitano ijayo CCM ina nia ya dhati ya kuongeza kasi ya maendeleo vijijinI,” amesema.

Wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM wakisoma vitabu vinavyoeleza Ilani mpya ya uchaguzi ya chama hicho kwa mwaka 2025-2030 wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo alipokuwa akiiwasilisha kwa wajumbe, jijini Dodoma leo Ijumaa Mei 30, 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi

Profesa Kitila amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa sehemu kubwa ya maoni ya ilani hiyo imetokana na maoni ya wanaCCM wananchi na wadau mbalimbali, makundi mbalimbali wakulima, wafugaji, wasanii.

“Ilani imeakisi matamanio na matarajio ya wananchi ni ilani ya Watanzania.Lengo la Ilani ya CCM 2025/2030 ni kukuza uchumi jumuishi na kuimarisha ustawi wa wananchi wote,” ames-ema Profesa Kitila ambaye ni mbunge wa Ubungo.

Profesa Kitila amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo, lengo la CCM ni kukuza kilimo kutoka asilimia 4.6 hadi 10 ifikapo 2030 huku ikianisha hatua 19 za kutekeleza lengo hilo.

Miongoni mwa hatua hizo ni kuendelea kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora na kwa bei nafuu, kutoa ruzuku za pembejeo ili kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima.

Nyingine ni kuboresha na kuongeza miundombinu ya umwagiliaji itakayongeza hekta za sasa kutoka 900,000 hadi milioni tano ifikapo 2030 ili kupunguza utegemezi wa kilimo cha mvua.

“Kuimarisha upatikanaji wa zana za kisasa za  kilimo kwa wakulima ikiwemo kusambaza matrekta 10,000 kwa wakulima. Kuanzia mfuko wa dhamana kupitia mfuko wa pembejeo za kilimo, benki ya maendeleo ya kilimo na ushirika ili kuwawezesha wakulima wengine,”

Katika kuhakikisha sekta hiyo, Profesa Kitila amesema ilani ya CCM itahakikisha Serikali inatunga na kutekeleza mikakati itakayohakikisha sekta ya viwanda inakua kwa asilimia tisa kwa mwaka kutoka sasa.

Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi akisoma moja ya kitabu cha Ilani mpya ya Uchaguzo ya chama hicho ilipokuwa ikiwasilishwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM jijini Dodoma leo ijumaa Mei 30, 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi

Profesa Kitila amesema Ilani imeanisha mikakati sita ya kukuza sekta ya viwanda ikiwemo kutunga na kutekeleza sera na sheria itakayozuia usafirishaji nje bidhaa zitakanazo na rasilimali za asili na mazao ikiwemo korosho na kahawa pasipo kuongezewa thamani.

“Kubuni na kutekeleza mkakati wa kuanzisha viwanda vya kimkakati ikiwemo viwanda vya kuzalisha madawa, chuma, mbolea, sukari, bidhaa za ngozi na mavazi kwa lengo la kujitosheleza kimahitaji,”

“Kuweka mazingira maalumu ya kuvutia ujenzi wa viwanda vidogo vijijini kwa lengo la kuongeza thamani ya awali katika sekta za kimkakati za kilimo, uvuvi, mifugo ili kuongeza fursa za ajira na kupunguza upotevu wa mazao,” amesema Kitila.

Related Posts