Wanandoa wauawa, Polisi yamsaka mtuhumiwa anayedaiwa kuwa mtoto wao

Moshi. Wanandoa Godfrey Mota (60) na Blandina Ngowi (53), wakazi wa Msufuni, Msaranga katika Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameuawa na mtu anayedaiwa kuwa mtoto wao wa kumzaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, ambapo amesema mauaji hayo yalitokea Mei 29, 2025 ndani ya nyumba ya kupanga waliyokuwa wanaishi familia hiyo eneo la Msufuni.

“Tukio hilo limetokea ndani ya nyumba ya kupanga waliyokuwa wakiishi wanandoa hao pamoja na kijana wao wa kiume (jina limehifadhiwa) ambaye ametoweka baada ya mauaji hayo kutokea,” amesema Kamanda Maigwa.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.

Related Posts