Mapya yaibuka waliomgombania Mwijaku, mmoja atupwa lupango

Dar es Salaam. Mmoja kati ya wanafunzi watatu kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, waliodaiwa kum-shambulia mwenzao wakimgombania msanii na mtangazaji wa vipindi vya redio, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku, ameswekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya jinai inayomkabili na wenzake hao.

Mwanafunzi huyo Mary Gervas Matogo-lo (22), mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Ma-hakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, leo Mei 30, 2025.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane ya kusababisha madhara kim-wili, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.

Mbali na Mary wanafunzi wengine wali-opandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo ni Ryner Ponci Mkwawili wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam na Asha Suleiman Juma, wana-funzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Sa-laam (Tia).

Awali kabla ya kupandishwa kizimbani leo, wanafunzi hao walikamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam baada ya kipande cha picha jongefu (clip) kusambaza mitandaoni Aprili 20, 2025 ikiwaonesha wakimfanyia udhalilishaji mwanafunzi huyo mwenzao.

Wanafunzi watatu Mary Matogolo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ryner Mkwawili wa Chuo cha Ardhi, Dar es Salaam na Asha Juma Chuo cha Uhasibu wakiwa katika Mahakama na Hakimu Kisutu leo Ijumaa Mei 30, 2025.

Pia Jeshi la Polisi lilimhoji Mwijaku baada ya kuhusishwa na tukio hilo, kutokana na kutajwa na wanafunzi hao katika video hiyo.

Wanafunzi hao wamepandishwa ki-zimbani mahakamani hapo na kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Tumaini Mafuru.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa wote wanadaiwa kula njama za kutenda uhalifu.

Katika shtaka hilo Wakili Mafuru amedai kuwa Machi 16, 2025 eneo la Sinza Wila-ya ya Ubungo, Dar es Salaam, washtaki-wa walikula njama kwa nia ya kutenda kosa ya kuchapisha taarifa za uongo.

Shtaka la pili ambalo ni kusabambaza taarifa za uongo linawakabili Mary na Asha.

Wanadaiwa kuwa siku hiyo walisambaza taarifa za uongo, katika mtandao wa WhatsApp yenye maneno kuwa, “Toa sauti umefanya mapenzi na Mwijaku lini na wapi”.

Shtaka la tatu ambalo pia ni kusambaza taarifa za uongo linalomkabili, Ryner peke yake.

Anadaiwa kuwa siku hiyo alisambaza taa-rifa hizo kupitia mtandao wa WhatsApp.

Shtaka la nne ambalo ni kusababisha madhara makubwa, linamkabili Mary peke yake, akidaiwa kuwa siku hiyo alimshambulia Magnificant Kimario kwa kumpiga kichwani na chuma na kumsab-abishia maumivu makali.

Shtaka la tano ambalo ni kusababisha madhara makubwa, ambalo linawakabili washitakiwa wote.

Wakili Mafuru amedai kuwa siku hiyo kwa kutumia nguvu, wamshtakiwa walimvuta nywele Magnificant na kusab-abisha madhara makubwa.

Shtaka la sita na saba, ambayo ni kuhari-bu mali, pia yanamkabili Mary peke yake.

Wakili Mafuru amedai kuwa siku hiyo Mary aliharibu laini ya simu na simu aina ya Samsung yenye thamani ya Sh700,000 mali ya Magnificant.

Shtaka la nane ni kutishia kuua, ambalo linawakabili washtakiwa wote, wakidai-wa kuwa siku hiyo walimtishia kumuua Magnificant kwa kutumia kisu.

Hata hivyo washtakiwa wote wamekana mashitaka hayo.

Upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo uko hatua za mwi-sho kukamilika, hivyo uliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Gwantwa, alitaja masharti ya dhamana, kuwa kila mshitakiwa ana-takiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho, vit-ambulisho vya Taifa, watakaotia wa-takaosaini Bondi ya dhamana ya Sh5 mil-ioni kila mdhamini.

Washtakiwa Ryner na Asha wametimiza masharti hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana lakini Mary ameshindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana.

Hivyo Hakimu Mwankuga ameamuru apelekewe mahabusu gerezani mpaka Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Related Posts