Afrika yajadili mbinu matumizi sahihi ya intaneti kukuza ajira kwa vijana

Dar es Salaam. Tanzania imesema iko tayari kushiriki katika uchumi wa kidijitaji na kuhakikisha inatimiza malengo ya milenia ya mageuzi ya teknolojia yaliyopo duniani, huku ikihamasisha vijana watumie intaneti kwa manufaa.

Kauli hiyo inakuja, huku viongozi mbalimba-li barani Afrika, wakitafuta mbinu za kuhakikisha vijana barani wanatumia fursa zilizopo kwenye mitandao, kukuza uchumi kidijitali na kuachana na matumizi yasiyofaa.

Viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo jinsi gani kupitia intaneti itaiinua zaidi Afrika, lakini pia kuwainua vijana wa bara hilo hasa katika kipindi hiki cha ukosefu wa ajira na kwamba huo unaweza kuwa mwarobaini, vijana kutafuta fursa  za masoko.

Akizundua kongamano la 14 la Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF) leo Ijumaa, Mei 30, 2025 kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema Tanzania iko tayari.

Amesema watu wengi katika nchi mbalim-bali za Afrika wanaoongoza kutumia mitandao ni vijana, akiwaasa watumie katika njia sahihi wasitumie katika maudhui yasiyofaa, bali katika kukuza uchumi wa kidigitali na kutafuta mbinu mbalimbali za masoko.

Amesema katika kuhakikisha Tanzania inatumia mtandao kwa manufaa, kumekuwa na mageuzi mbalimbali ya kidijitali nchini.

“Mfano Serikali inayoongozwa na Rais Sa-mia Suluhu Hassan, kwa sasa imeendelea kufanya mageuzi mbalimbali ya kidijitali ikiwemo kuanzishwa masomo ya ubunifu, kuanzia shule za elimu ya awali mpaka elimu ya juu lengo lake ikiwa kuchochea mageuzi ya kidijitali,” amesema.

Pia amesema kwa sasa mtandao ni muhimu katika utoaji wa huduma mbalimbali iki-wemo maji, nishati ya umeme na nyingine-zo na ndiyo maana Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti katika mageuzi ya kidijitali.

Vilevile amesema serikali imeendelea ku-hamasisha na kuboresha mazingira ya kidi-jitali mijini na vijijini.

Silaa amesema jukwaa hilo ni muhimu kwa maendeleo ya teknolojia afrika na dunia kwa ujumla, hivyo Tanzania kuandaa mtandao huu ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuchochea mageuzi ya kidijitali.

Amesema matumizi ya intaneti kwa wana-wake na wanaume kwa mjini na vijijini, yamepanda hivyo lazima juhudi ziongezwe ili kuongeza matumizi hayo hasa maeneo ya vijijini.

“Kwa kuliona hili, Tanzania pia tumewekeza zaidi vituo vya Tehama ambavyo vitaibua fursa za mafunzo kwa vijana na kupitia hivyo vituo vijana watajua intaneti, namna ya kuitumia. Kwa sasa Tanzania ina vituo nane ambavyo vipo chini ya Tume ya Te-hama,  kwa ajili ya kuwanoa vijana kidijita-li,” amesema Silaa.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mohammed Hamis Abdulla amesema jitihada kubwa zimefanyika katika kukuza dijitali nchini, ikiwemo kuhamasisha uchumi wa kidijitali, serikali imefanya jitihada kubwa.

“Mapinduzi ya kidijitali yana umuhimu mkubwa katika jamii ya Afrika ambayo ya-naambatana na athari mbalimbali ikiwemo uhalifu wa mitandaoni, hivyo ndiyo maana tunaungana pamoja kuona namna ya ku-hamasisha usalama,” amesema.

Amesema kuwa mkutano huo utaandaa Af-rika ya baadae ambayo inatakiwa kuwa na maendeleo makubwa ya uchumi wa kidijita-li, na ili kufika huko ni lazima iungane katika kuchochea mageuzi hayo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Mtandao wa AfIGF, Alhagie Mbow amedadavua kauli mbiu isemayo kuelekeza mustakabali wa kidijitali wa Afrika kwa utawala jumuishi, ustahimilivu, ubunifu na usawa.

Amesema hiyo ni kauli mbiu ambayo ina taswira ya hali halisi kwa Afrika, hivyo ina-takiwa kuchukua hatua, inadhihirisha kwamba kwa sasa Afrika si mtazamaji tena wa mtandao kiwango kilikuwa chini lakini kwa sasa ni mtendaji.

“Kwa hali ilivyo kwa sasa uchumi wa kidi-jitali unaokua kwa kasi unawalenga zaidi vi-jana, lakini bado kuna pengo la usawa kati ya mwanamke na mwanaume hiyo pia ni changamoto, lakini changamoto nyingine ni miundombinu bado kuna maeneo haijafi-ka,” ameeleza na kuongeza;

“Pia kuna makundi ya vijana yaliyotengwa ambayo hayafikiwi na hiyo huduma.”

Pia Mbow akahamasisha kujenga na kuwepo kwa wingi wa shule na vituo vina-vyofundisha ubunifu na kwamba hivyo vitakuwa chachu kwa Afrika kuwa kama nchi zingine zilizoendelea.

Amemalizia kuwa sisi Waafrika tuna uwezo wa kuamua tupige hatua gani katika ma-tumizi ya kidijitali hatma ipo mikononi mwetu lazima tuchukue hatua katika Afrika bora na yenye maendeleo.

Related Posts