KESI YA TUNDU LISSU YASOGEZWA MBELE

………………

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya Jinai inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA, Tundu Lissu hadi Juni 16, 2025, na kuagiza aendelee kushikiliwa rumande.

Uamuzi huo umetolewa leo baada ya shauri hilo kutajwa mahakamani, ambapo upande wa Jamhuri uliomba muda zaidi wa upelelezi kukamilika.

Ikumbukwe kuwa Lissu anakabiliwa na mashtaka mbalimbali, huku kesi hiyo ikifuatiliwa kwa karibu na umma kupitia matangazo ya moja kwa moja.

Nje ya Mahakama Wakili
wa Upande wa Utetezi katika Kesi ya Uhaini namba 8607/2025, inayomkabili
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu dhidi ya
Jamhuri, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema mahakama imeonya na kuamuru pande zote
mbili kuacha kutoa kauli zinazoashiria kudharauliwa kwa mahakama, pindi
mahakama hiyo inapokuwa imeshakaa.



Related Posts