Dar es Salaam. Wanasiasa wawili waliokuwa sehemu ya kundi la G55 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Emmanuel Ntobi na Glory Tausi, wamejiunga na ACT Wazalendo.
Hatua ya wawili hao kutimkia ACT- Wazalendo inakuja wiki mbili tangu wanamuungano wenzao wa G55, walipotangaza kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma).
Akizungumza baada ya hatua hiyo leo, Jumanne, Juni 3, 2025, Glory amesema anafurahishwa na namna chama hicho kinavyolinda, kujali na kuthamini usawa wa jinsia.

Kwa upande wa Ntobi, amesema chama hicho kimeweka wazi mpango wa kushiriki uchaguzi, amekiona kuwa jukwaa sahihi kwake, kwa kile alichoeleza, ‘muhuni hasusiwi.’
Wawili hao wamekabidhiwa kadi na Katiba za chama hicho na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu.
Awali, Ntobi alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga, kabla ya kusimamishwa kwa kile kilichodaiwa kuwa alifanya kosa la utovu wa nidhamu.
Kwa upande wa Glory, ndiye mwanzilishi wa programu ya Chadema Digital na aligombea nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.
Endelea kufuatilia Mwananchi.