Aliyekuwa muasisi wa Chaumma atimkia Chadema

Dar es Salaam. Aliyekuwa mmoja wa waasisi wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Eugene Kabendera leo Jumatano, Juni 4, 2025 ametangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kabendera ametambulishwa mbele ya waandishi wa habari na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Aman Golugwa, makao makuu ya Chadema, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

“Ametuonesha utayari wa kuyasema yaliyomjaa moyoni mwake,” amesema Golugwa.

Kabendera ameishukuru Chaumma kwa nafasi waliyompa katika kipindi chote akiwa huko na sasa ameamua kuhamia Chadema, baada ya kuona mwelekeo wa chama hicho umebadilika.

Related Posts