Dodoma. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimemaliza kimepata rais mpya, Suleiman Ikomba, aliyeibuka mshindi kwa kupata kura 608 dhidi ya kura 260 alizopata aliyekuwa rais wa awamu iliyopita, Leah Ulaya. Kura moja iliharibika, na kufanya jumla ya kura zilizopigwa kufikia 869.
Uchaguzi huo umefanyika jana usiku na mshindi amepatikana leo asubuhi Juni 10, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma.
Uchaguzi huo umehusisha wajumbe wote wa CWT kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Ikomba aliwataka wanachama wa CWT kuweka kando tofauti na makundi ya uchaguzi, na badala yake kushikamana kwa ajili ya kujenga chama imara na chenye mshikamano.
“Kwanza tuwashukuru sana. Uchaguzi tumemaliza salama. Hivyo mimi niwaombe tumalize makundi ambayo tuliyoyatengeneza katika uchaguzi, ila sasa tumemaliza na makundi nayo tuyamalize,” alisema Ikomba.
Endelea kufuatilia Mwananchi.