……………………….
Naibu wa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Khamis Hamza Khamis amewataka wananchi wanaofanya shughuli kwenye fukwe
kutoharibu mazingira na badala yake wafuate sheria ikiwemo kutotupa taka ovyo.
Ametoa wito huo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Asya Mwadini Mohammed aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa
kusimamia utunzaji wa mazingira ya fukwe.
Akiendelea
kujibu swali hilo, Naibu Waziri Khamis amesema kuwa Serikali inaendelea kuchkua hatua za kusimamia
sheria ambayo inawataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya
mita 6o kando mwa vyanzo vya maji.
”Ni kweli kuna baadhi ya shughuli
zinafanyika kwenye kingo za bahari, kingo za mito na hata kingo za mawiwa
ambayo ni vyanzo vya maji vinavyosaidia shughuli za kiuchumi na sasa zipo hatua
ambazo Serikali tumezichukua ikiwemo usimamizi wa sheria na kutoa elimu,” alisema.
Aidha, Mhe. Khamis alisema Serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana Mamlaka ya Hifadhi ya Mlima
Kilimanjaro (KINAPA) itaendelea kupambana na vitendo vya uharibifu wa mazingira
katika Mlima Kilimanjaro vikiwemo uchomaji wa moto.
Alisema hayo wakati akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Shally Raymond aliyetaka kufahamu Serikali ina
moango gani wa kuhakikisha theluji ya Mlima Kilimanjaro ambayo ni kivutio cha
utalii haiyeyuki.
Mhe. Khamis alisema Serikali itaendelea
kutumia sheria, miongozo, kanuni na kampeni ambazo zina maelekezo ya mbalimbali
ya utunzaji wa vyanzo uvya maji, upandaji miti, kuhamasisha matumizi ya nishati
safi ya kupikia.
Awali, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Esther Malleko lililoulizwa
kwa niaba yake na Mhe. Shally kuhusu Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu wa mazingira
unaotokana na shughuli za kibinadamu, Mhe. Khamis alisema
uharibifu wa mazingira
unaotokana na shughuli za kibinadamu unatokea katika sekta nyingi nchini.
Hivyo, alisema ili kudhibiti uharibifu
huo, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuandaa Sera,
Sheria kanuni mikakati na miongozo mbalimbali inayobainisha hatua zinazochukuliwa
kukabiliana na changamoto hizo.
Alitaja Sera ya Taifa ya Uhifadhi wa
Mazingira ya 2021, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191 ikisomwa pamoja na
marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na.5/2025 na Mpango Kabambe wa
Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) ni hatua zilizochukuliwa.
Naibu Waziri Khamis aliongeza kuwa
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kwa wananchi
kuhusu uhifadhi wa mazingira na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa njia
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari, ziara za viongozi na mafunzo
mashuleni