Leo tarehe 10 Juni 2025 Kamati ya Pamoja ya Wataalamu ya Uimarishaji Mpaka wa Tanzania na Rwanda (JTC) imetembelea eneo la mto Kagera lililopo wilayani Ngara mkoa wa Kagera ikiwa ni sehemu ya mpaka wa kimataifa.
Eneo hilo la mto Kagera lililotembelewa ni sehemu ya mpaka wa kimataifa unaotenganisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi maarufu kama mafiga matatu pamoja na eneo la RUSUMO.
Uamuzi wa kutembelea maeneo hayo mawili ni sehemu ya programu ya kikao cha JTC kinachoendelea katika mji wa Ngara mkoani Kigera.