Moto wateketeza maduka Chato | Mwananchi

Geita. Maduka zaidi ya 17 katika eneo la Buseresere wilayani Chato, Mkoa wa Geita yameteketea kwa moto ambao chanzo chake hakijafahamika.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Hamis Dawa amethibitisha kutokea kwa moto huo akisema taarifa zaidi atazitoa muda mfupi ujao.

Kwa mujibu wa mashuhuda moto huo ulizuka saa tatu usiku ambapo wamedai ulianza kwenye duka moja linalouza vifaa vya umeme kabla ya kusambaa kwenye maduka mengine na kusababisha uharibifu wa mali.

Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka hayo wamelalamikia kuchelewa kwa gari la zimamoto hivyo moto kusambaa zaidi na kusababisha hasara.

Moto huo umefanikiwa kuzimwa na wananchi wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto.

Endelea kutufuatilia Mwananchi.

Related Posts