:::::
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikina na Taasisi ya Fountain Gate academy leo wameingia makubaliano ya ushirikiano kwaajili ya upimaji wa afya ya wanafunzi ambao wanashiriki michezo.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya JKCI kuigia mkataba wa ushirikiano kama huo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya kuwapima wachezaji afya kabla ya kufanya mazoezi au kucheza.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini mkataba huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI,Dk Angella Muhozya amesema
lengo ni kusaidia watoto ambao Fountain gate wanawajenga katika michezo.
“Tunawapongeza sana Fountain gate academy kwa kulitambua hili wana shule 14 na wanafanya michezo wanawajali wanamichezo hongera sana.
Amesema programu ya Moyo wa Michezo “Sports Cardiology) ni programu mpya JKCI na wameanzisha ili kulinda wanamichezo wa kupima afya na kitengo hicho ni maalumu kumsaidia mtu anayefanya michezo ana afya inayoweza kumsaidia kufanya michezo.
Dk Muhozya amebainisha kuwa wamelenga kuleta kinga kwa kuzuia magonjwa ya moyo kwa wanamichezo amba watatoa vipomo na elimu ya masuala ya afya katika michezo.
“Nyie ni wadau muhimu karibuni na wakati mwingine wanafunzi mnawahamasisha wapende michezo kwa kufanya hili,”amesisitiza Dk Muhozya.
Kwa upande Rais wa Fountain Gate Academy leo,Japhet Makau amesema kusudi lao ni watoto wanakuwa na afya njema na wanapenda michezo.
“Zaidi ya elimu tumejikita kwenye michezo kuna programu ya vijana wa chini ya miaka mitano wanajifunza na kufundishwa michezo tuna timu ya chini ya miaka saba na tuna vijana chini ya miaka 17,tuna timu inashiriki lingi kuu ya Tanzania ya wasichana na inafanya vizuri, tuna timu ya Fountain Gate ambayo inacheza mpira wa miguu.
Amesema wana zaidi ya vijana 10,000 katika taasisi yao waliojikita kwenye michezo na kwa miaka yote hawakuwa na utaratibu wa kuchunguza afya japo hawajapata janga.
“JKCI imekuja muda muafaka kuna vijana wengi wanataka kujiendeleza kimichezo tunataka wapime afya zao katika shule zetu 14 ,naamini vijana wote watakuwa na nafasi ya kufanya uchunguzi wa moyo tumekimbialia kwa haraka baada ya kuona jambo hili ni muhimu.
Ameongeza”Kabla hajaingia kwenye michezo kwanza tujue afya yake na hata fanya mazoezi yasioyendana na afya,tunawahakikishi wazazi kuwa watoto wanaocheza watakuwa na afya zinazoruhusu hawa baadae wanatamani kuwa madaktari tunataka wanafunzi wafundishwe baadae wawe madaktari watakaosaidia katika eneo hili .
Naye Salome Jovin ambaye ni mwanafunzi amesema Sports cardiologist inamanufaa makubwa kwasababu afya ya mwili ni kila kitu hivyo itawasaidia na wanaishukuru JKCI kwa kuungana nao.
“Kuna manufaa mengi yasiyoisha na tunajua michezo ni kila kitu hivyo kutokana na hili michezo katika shule yetu itaenda vizuri,”amesisitiza.
Mwishooo…