MADINI YAMEVUKA LENGO LA SERA KABLA YA MUDA

::::::::

Waziri wa Madini Anton Mavunde amesema kuwa sekta ya madini Nchini imepiga hatua kubwa ya kihistoria kwa kufikia mchango wa asilimia 10.1 katika pato la taifa wa mwaka 2024 ikiwa nimwaka mmoja kabla la lengo la asilimia kumi lililowekwa kwenye sera ya madini yam waka 2009

Mavunde ameyasema hayo katika ufunguzi wa jukwaa la nne la ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini ambapo pia ameiagiza tume ya madini kupitia kanuni zitakazowawezesha wazawa kupata fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya madini

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume ya madini dkt Janeth Lekashingo amesema ushirikishwaji wa watanzania kwenye fursa za uwekezaji umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka

Akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa mwanza, mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan masala amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuleta tija kwa wawekezaji kwenye seta ya madini







 

Related Posts